Home BUSINESS WACHIMBAJI WADOGO IGALULA WAMLILIA WAZIRI KUPELEKA UMEME MGODINI

WACHIMBAJI WADOGO IGALULA WAMLILIA WAZIRI KUPELEKA UMEME MGODINI

 
Mashine ya kufua Umeme inayotumia mafuta ya dizeli Ambayo hutumiwa na wachimbaji wadogo katika mgodi wa Igalula uliopo wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita.

Na:Saimon Mghendi, Nyang’hwale – 29,November,2021

WACHIMBAJI wadogo wa Dhahabu katika Mgodi wa  Igalula Gold Mine  uliopo Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita wamemuomba Waziri wa nishati  Januari Makamba kufikisha  huduma ya nishati ya umeme kwenye mgodi wao ili kupunguza gharama kubwa za mafuta.

Mkurugenzi wa mgodi huo Jumanne Misungwi ametoa ombi hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mgodini hapo na kubainisha kuwa iwapo serikali itawapelekea huduma hiyo utarahisisha utendaji wa shughuli za uzalishaji wa Madini ya Dhahabu.

“Tunaiomba serekali kupita Waziri mwenye zamana husika kutuletea huduma ya umeme hapa mgodini kwetu ili tuweze kufanya kazi kwa ufanisi na kupunguza gharama tunazoptumia kwa kununua mafuta”,alifafanua Misungwi.

Kwa upande wake meneja wa mgodi alisema kuwa mgodi huo una mialo ya kuoshea dhahabu zaidi 400 hivyo gharama za uzalishaji zinazotumika ni kubwa kwakua mitambo yao uzalishaji inatumia mafuta badala ya umeme jambo ambalo linawatia hasara ukilinganisha na kupanda kwa mafuta hayo.

Aidha meneja huyo ameeleza kuwa mgodi wake umekuwa ukichangia shughuli mbalimbali za maendeleo pamoja na kutengeneza miundombinu ya barabara ili kurahisisha ubebaji wa mawe yanayosadikiwa kuwa na Madini ya dhahabu kupelekwa kwenye mitambo wa kuchenjulia.

Hata hivyo Mgodi huo umekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Nyang’hwale kwa kutoa ajira zaidi ya 6000 huku wachimbaji wadogo nao wakisisitiza serkalikusikia kilio chao na kuwasogezea huduma ya umeme ili waweze kujiongezea kipato Pamoja na serikali kwa ujumla.

“Kwakweli changamoto kubwa hapa katika Mgodi huu ni umeme nyie wenyewe mmeona tunatumia majenereta na bei ya mafuta ni kubwa sana kama serekali itasikia kilio chetu na kutuletea huduma hiyo tutafanya kazi kwa ufanisi Zaidi”,Alisisitiza Abduli Zuberi ambaye ni mchimbaji mdogo wa Mgodi wa Igalula.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here