Home LOCAL UWT NJOMBE YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA HOTUBA NZURI SCOTLAND

UWT NJOMBE YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA HOTUBA NZURI SCOTLAND

Na: Mwandishi wetu.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Njombe  Scolastika Kevela amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na hotuba yake nzuri mbele ya mkutano wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukizungumzia Mabadiliko ya Tabianchi (COP).

Katika hotuba yake hiyo iliyojaa hisia na umakini mkubwa imetafsiriwa na magwiji wa diplomasia kuwa ililenga kuyabeba mataifa yote ya Afrika huku akiongea kwa ujasiri mkubwa akitumia nafasi hiyo nchi tajiri ambazo nyingi zinaongoza kwa kuchafua hali ya hewa ziwajibike zaidi katika vita hiyo.

Akizungumzia hatua hiyo Scolastika ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ‘Udalali ya Yono Auction Mart’ alisema hotuba ya Rais Samia siyo tu imeibeba Tanzania bali Bara zima la Afrika na kutokana na changamoto mbalimbali za halo ya mabadiliko ya tabia nchi inazozikabili nchi hizo.

“Kwa niaba yangu, UWT Mkoa wa Njombe na wanawake wenzangu nchi nzima napenda kutumia fursa hii kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua yake ya kuliwakilisha vyema Taifa mbele ya wajumbe wa Mkutano wa umoja wa mataifa, hii ni hatua kubwa kwa nchi yetu” 

“Rais Samia, hakupepesa macho, zaidi alisisitiza kuwa nchi tajiri sasa ziwajibike zaidi kwa kufadhili miradi ya kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi katika nchi zinazoendelea akimaanisha nchi zetu za Afrika” alisema Scolastika

Alisema kauli ya Rais Samia kugusia hali ya chafuzi  wa hali ya hewa, ambao sasa unatishia kutokea kwa milipuko ya magonjwa, ukame, njaa na mafuriko, unachangiwa sana na nchi tajiri tokana na nchi hizo kuwa na viwanda vingi vikubwa vinavyozalisha hewa chafu.

“Hii inanikumbusha ujasiri wa mwalimu Nyerere kwa nchi tajiri na ikafikia nchi za Afrika zinamtegemea yeye azisemee kwenye mambo mengi. Nyerere hakuwa anaogopa kuwaambia ukweli mbele zao, mfano aliwalaumu sana Waingereza kwa kuungana na makaburu wa Afrika Kusini miaka ya 1990” aliongeza Scolastika.

Aidha alisema ni dhahiri kuwa Rais Samia alikuwa anaweka msingi wa ushirikiano wote wa kimataifa kuhusu mabadiliko hayo ya tabianchi kwa nchi za Afrika na hiyo ni kwa sababu COP26 ndicho chombo kikuu cha kufanya maamuzi cha kutekeleza Mkataba na vyombo vya ufuatiliaji katika masuala ya hali ya hewa.

Katibu Mkuu huyo wa UDP alisema ushiriki wa Rais Samia katika mkutano huo ulikuwa ni wa muhimu kwani yeye ni kinara katika masuala yatabia nchi, ajenda ambayo huipigia chapuo kila apatapo nafasi katika majukwaa nmbalimbali. 

“Mathalani, akihutubia Mkutano Mkuu wa 76 wa UN, Rais Samia alijikita katika kuiomba Dunia kuelekeza nguvu zake katika masuala ya tabianchi na baada ya hatua hiyo nchi nyingi za Kiafrika zilijitokeza kuunga mkono hoja yake” alisisitiza Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Yono.

MWISHO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here