Home BUSINESS TWCC YAZINDUA MRADI KUWAWEZESHA WABUNIFU WA MITINDO NA MAVAZI DAR.

TWCC YAZINDUA MRADI KUWAWEZESHA WABUNIFU WA MITINDO NA MAVAZI DAR.




Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania TWCC amewataka Wanawake wajasiriamali waliopa fursa ya kushiriki kwenye mradi maalum wa ubunifu wa mitindo na mavazi kuitumia vizuri fursa hiyo kuboresha biashara zao ili kuweza kuyafikia masoko makubwa ndani na nje ya nchi.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa kuwajengea uwezo wanawake kwenye Sekta ya nguo na ubunifu wa mavazi (Fashion for Change Project), unaowezeshwa kwa ufadhili wa Shirika la Kijerumani la GIZ na kuratibiwa na TWCC ambapo  amewataka wabunifu hao kushirikiana kwa pamoja katika kazi zao na kuboresha biashara zao ili ziweze kushindana kitaifa na kimataifa.

Amesema kuwa kwa sasa Sekta hiyo imekuwa sana kutokana na namna ambavyo wabunifu na washonaji kujiendeleza na kubuni aina mbalimbali za mitindo jambo lililoifanya jamii kupenda kazi zao na kuzitumia. “Nitoe wito kwa wanawake Wajasiriamali ambao mmepata nafasi ya kushiriki katika program hii kutumia vizuri nafasi mlioipata ili kuweza kuboresha biashara zenu ziweze kushindana kitaifa na kimataifa” Amesma Mercy Silla

Ameongeza kuwa TWCC inaamini kuwa kwa kufanya hivyo wanaweza kupata Masoko ya uhakika na hasa Soko la AGOA ambalo linatoa fursa ya kuuza bidhaa Marekani.

“Ni matarajio yangu kuwa mradi huu unakwenda kuwaonesha njia ili nasi Tanzania tuweze kupata wanawake wengi wanaonufaika kwa kuuza bidhaa zao kwenye soko la AGOA pamoja na masoko mengine ya Kitaifa  na kimataifa” Ameongeza Mercy Silla.

Kwa upande wake Mwakilishi wa GIZ Business Scouts for Development, Lydia Koch ameipongeza TWCC kwa kuweza kusimamia program hiyo na kwamba Shirika lao litaendelea kuunga  mkono juhudi za Serikali za kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuetaendelea kushirikiana na TWCC kwa kuiwezesha ili kuwafikia wanawake wengi zaidi.
“Mradi huu unalenga kusaidia Sekta ya nguo na ubunifu wa mavazi hivyo wanawake hawa wataweza kupata mafunzo ili kuwasaidia kwenye shughuli zao na biashara zao kwa ujumla, pia ni mradi endelevu ambao mwakani utawafikia wanawake wengi zaidi” Amesema Koch.

Akizungumza alipokuwa akihitimisha hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Mwajuma Hamza amesema kuwa Taasisi hiyo imeanza kufanyakazi kupitia kongani ikiwa ni kuhakikisha wanawake walio kwenye Sekta kama hizo wanafikiwa na kusaidiwa kwa kuwajengea uwezo  ili kufikia malengo yao.
“Kwa sasa tumeweza kuwajengea uwezo wanawake 35 ambao wametoka kwenye mikoa mbalimbali kwa kupitia mchakato wa kuwapata ambao ulifanyika kuweza kuwafikia na kuwasaidia kitengeneza mtandao wa  kitaifa katika Sekta hii utakaowasaidia kuwaleta kwa pamoj na kushirikiana ili kupata masoko ya pamoja” Ameongeza Mwajuma.

TWCC ni Chama cha Wafanyabiashara wanake Tanzania kinachofanya kazi na wanawake kutoka Sekta zote na mikoa yote Bara na Visiwani yenye wanachama zaidi ya elfu 10 na kuwawezesha kiuchumi wanawake zaidi ya elfu 20 nchini.

Mwisho.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here