Home BUSINESS TUME YA MADINI MBOGWE IMEKUSANYA ZAIDI BILIONI 6 KWA MIEZI MINNE

TUME YA MADINI MBOGWE IMEKUSANYA ZAIDI BILIONI 6 KWA MIEZI MINNE



Afisa Madini Mkazi wa Mkoa mpya wa kimadini Mbogwe, Muhandisi Joseph Kumbur


Na: Saimon Mghendi, MBOGWE.

TUME ya madini katika Mkoa mpya wa kimadini Mbogwe imesema kuwa imefanikiwa kukusanya Zaidi ya bilioni sita kwa muda wa miezi minne jambo ambalo ni mafanikio makubwa kufanywa na ofisi hiyo licha ya kuwa bado ina muda mchache toka ianzishwe.

Hayo yalibainishwa novemba 6 na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa mpya wa kimadini Mbogwe, Muhandisi Joseph Kumburu, katika semina iliyofanyika katika Mgodi wa wachimbaji wadogo wa Isanjabadugu uliopo kata ya Nyakafulu wilayani Mbogwe, Semina iliyo lenga kuwapa wachimbaji wadogo elimu.

Awali Katibu wa Mgodi wa IsanjabaduguPatrick Basoga alisema kuwa mara baada ya Tume ya madini Kupitia kwa Afisa madini Muhandisi Joseph Kumburu, kuisambaratisha safu ya uongozi iliyokuwepo  awali mgodi huo umekua ukifanya kazi kwa mafanikio makubwa.

Katika hatua nyingine Muhandisi Kumburu ameeleza utaratibu mpya uliopelekea kuongezeka kwa kodi ya serikali Pamoja na kutumia fursa hiyo kuwaonya watu wachache ambao bado sio waaminifu wanaotorosha madini ya dhahabu kupitia kwenye mialo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here