Home SPORTS TMDA YAANZA VIZURI MASHINDANO YA SHIMUTA

TMDA YAANZA VIZURI MASHINDANO YA SHIMUTA

wachezaji timu ya wanawake ya TMDA katika mpira wa Netball wakiwa katika picha ya pamoja.


Wachezaji wa timu ya Mpira wa Miguu ya TMDA wakiwa katika picha ya pamoja.

Wakati mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma,Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania(SHIMMUTA) yakiendelea Mkoani Morogoro, timu ya mpira wa miguu ya TMDA imeipa kipigo cha goli 1-0 timu ya Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) katika mechi iliyofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Mzinga tarehe 15 Novemba 2021.

Goli hilo lililofugwa na mchezaji wa TMDA Bw. William Swago limeipa mwanzo mzuri Mamlaka katika mashindano hayo.
Timu ya mpira wa pete TMDA Queens inatarajia kupambana na timu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kesho kwenye viwanja vya Magadu.

Mashindano haya yalianza tarehe 13 na yanatarajiwa kuisha tarehe 27 Novemba 2021

Timu ya Mpira wa Miguu ya TMDA ikiwa katika picha ya pamoja.   

Wachezaji wa timu ya Netball ya TMDA wakisali kabla ya kuanza mchezo wao katika mashindano ya SHIMUTA.

Credit – Fullshangwe Blog.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here