Home LOCAL TEMDO YAIOKOA SEKTA YA AFYA KWA KUTENGENEZA VIFAA TIBA BORA NA IMARA

TEMDO YAIOKOA SEKTA YA AFYA KWA KUTENGENEZA VIFAA TIBA BORA NA IMARA

Dkt. Sigisbert Mmasi, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko, Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO) akiongea na waandishi wa habari katika maonesho yalienda sambamba na wiki ya magonjwa yasiyoambukiza yanayoendelea mkoani Arusha.

Baadhi ya vifaa tiba vinavyotengenezwa na tasisi ya TEMDO  ambapo katika picha ni vitandanda vya kawaida vya kulalia wagonjwa na kitanda cha kujifungulia wanawake.
 
NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO) imetambulisha bidhaa za vifaa tiba 6 kati ya 16 walivyoanza kuvitengeneza tangu September 2021 lengo likiwa ni kuisaidia sekta ya afya na serikali kwa ujumla kupata bidhaa hizo kwa urahisi, kwa  gharama nafuu  na zenye ubora na uimara mkubwa tofauti na kuagiza vifaa hivyo kutoka nje ya nchi.

Akiongea na waandishi wa habari Dkt. Sigisbert Mmasi, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko, Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO) alisema kuwa taasisi hiyo ipo chini ya wizara ya viwanda na ilianzishwa ili kusaidia viwanda vikubwa vidogo na vya kati kwa kubuni mashine kwaajili ya kusaidia uchumi wa viwanda.

“Tumekuwa tukitengeneza mitambo mbalimbali kwaajili ya sekta ya kilimo vya kuongeza thamani kwenye mazao lakini pia tumetengeneza bidhaa kwaajili ya sekta ya Nishati na  sasa tumeanza kutengeneza vifaa tiba kwaajili ya sekta ya afya ambapo kwa kipindi cha miaka 10  tumekuwa tukitengeneza kiteketezi cha ambacho ni maalum kwa kuchoma taka zinazozalishwa hosipitali pamoja majokofu ya kuhifadhia miili na  kwanzia September mwaka huu tumeanza kutengeneza bidhaa nyingine,” Alisema Dkt Mmasi.

Dkt Mmasi alieleza kuwa bidhaa hizo 16  walivyovidizain walioanza kufanya ubunifu Julai 2021 baada ya kuona serikali inatumia fedha nyingi kuagiza vifaa tiba kutoka nje ya nchi ambapo kwanzia September  2021 walianza kutengeneza vifaa hivyo ambavyo baadhi take vitandanda vya kujifungulia wanawake,vitanda vya kawaida vya kulalia wagonjwa, vitanda vya madaktari vya kuchunguza wagonjwa, vifaa vya kuhifadhia vitu vya wagonjwa pamoja na vifaa vya kutundikia dripu.

Alifafanua kuwa  wanategemea mpaka itakapoisha mwaka wa fedha Julai 2022 watakuwa wanetengeneza vifaa tiba vya aina 17 na lengo no kurahisisha upatikanaji wa vifaa hivyo hapa nchini kwaajili ya hosipitali za serika na binafsi ambapo pamoja na vifaa hivyo kuwa sokoni kwa chini ya miezi mitatu wameona muamko mkubwa wa sekta hiyo kuhitaji vifaa hivyo.

“Tumeshiriki kwenye maonesho haya ili kuweza kujitangaza zaidi kwani nu fursa ya kufanya vifaa hivi bora na imara vitambulike na kujua ni waoi vinavyopatikana kwa bei nafuu lakini Ni vifaa ambavyo vinaweza kutengenezwa kwa urahisi pale vinapoharibika,” Alisema.

Alisema hosipitali nyingi na wadau wa afya hawajajua kuwa bidhaa hizo zinatengezwa TEMDO ndio mana tunazitangaza ambapo  maonesho hayo ni ya kwanza taasisi hiyo kushiriki ikiwa na vifaa tiba na tumeona mwitikio na mahitaji kwenye hosipitali ni makubwa kutokana na awali kuagiza kwa gharama kubwa nje ya nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here