Home SPORTS TANZANITE YAICHAPA DJIBOUTI 8-0

TANZANITE YAICHAPA DJIBOUTI 8-0




Na: Stella Kessy.

TIMU ya Tanzanite leo imemalizia hasira zake kwa Djibouti kwa kuitandika 8-0 katika mechi yake ya mwisho ya michuano ya  CECAFA wanawake U20 Uwanja wa FTC Njeru nchini Uganda.

Mabao ya Tanzanite leo yamefungwa na Aisha Masaka saba dakika ya tatu, 27, 60, 66, 72, 73 na 86  na lingine Clara Luvanga dakika ya 43.

Mechi nne za awali, Tanzanite ilishinda mbili 1-0 dhidi ya Eritrea na 3-2 dhidi ya Burundi na pia ilifungwa mbili, 1-0 na wenyeji, Uganda na 2-1 na Ethiopia.

Kwa matokeo hayo, Tanzanite inamaliza nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa, Uganda na Ethiopia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here