Home SPORTS TANZANITE YAICHAPA 3-2 BURUNDI CECAFA

TANZANITE YAICHAPA 3-2 BURUNDI CECAFA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!
TANZANIA imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya  CECAFA wanawake chini ya umri wa miaka 20 baada ya kuichapa Burundi 3-2 leo Uwanja wa FTC Njeru nchini Uganda

Mabao ya Tanzanite leo yamefungwa na Mwamvua Haruna dakika ya 60 kwa penalti, Clara Luvanga dakika ya 80 na Emiliana Isaya dakika ya 83.
Tanzanite iliyoshunda 1-0 dhidi ya Eritrea Jumamosi bao pekee la Clara Luvanga dakika ya 90 – itashuka tena dimbani Jumatano kumenyana na Ethiopia, kabla ya kuivaa Uganda Jumamosi na kukamilisha mechi zake kwa kucheza na Djibouti Novemba 9.