Home SPORTS TANZANIA YAANZA VIZURI CANAF 2021, YAIKANDAMIZA MOROCCO 2-1

TANZANIA YAANZA VIZURI CANAF 2021, YAIKANDAMIZA MOROCCO 2-1



Na: John Mapepele, WUSM

Timu ya Tanzania ya soka kwa wanaume kwa wenye ulemavu Tembo Warriors imeanza vizuri mashindano ya Afrika ya Mpira wa Miguu kwa Watu Wenye Ulemavu barani Afrika (CANAF 2021) baada ya kuibamiza vibaya mabao 2-1 timu ya Morocco katika mchezo wa ufunguzi uliofanyika leo Novemba 27,2021 uliofanyika  jijini Dar es Salaam.

Timu ya Morocco ilianza kushinda goli la kwanza katika sekunde ya 18 ya mwanzo kupitia kwa mshambuliaji wake  Chaamoun Redouane huku magoli ya Tanzania yakianza kufungwa kwenye dakika 15 kipindi cha pili na mshambuliaji  Alfani Kiangi wakati bao la ushindi likishindiliwa na Nahodha wa Tembo  Juma kidevu na kuifanya Tanzania kuibuka kidedea. 

Hata hivyo timu ya Tanzania imekosa magoli mengi licha ya kuwa imeonesha kiwango kikubwa uwanjani ukilinganisha na Morocco. 

Timu ya Tembo iliingia uwanjani ikiwa na ari kubwa huku ikishangiliwa na washabiki waliojitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Uhuru hali iliyoonyesha wazi kuwa ushindi ni lazima.

Katika hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa alisisitiza kuwa timu ya Tembo inakwenda kufanya vizuri kutokana na maandalizi kabambe  iliyofanya kwa  usimamizi wa Serikali.

Awali, Novemba 25, 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kupitia kwa Waziri Mkuu aliitakia kila la kheri timu hiyo na kuizawadia shilingi Milioni 150   ilizisaidie maandalizi ya mashindano hayo.

Previous articleMHE. BASHUNGWA AFUNGUA RASMI MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU KWA WENYE ULEMAVU (Canaf)
Next articleNAMUNGO FC YACHEZEA KICHAPO 3-1 MBELE YA PRISONS
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here