TIMU ya soka la ufukweni ya Tanzania leo inashuka dimbani kuchuna na Msumbiji katika fainali ya mashindano ya COSAFA yanayofanyika Durban, Afrika Kusini.
Katika michuano hiyo hatua ya kwanza Tanzania ilicheza na Msumbiji na kupata matokeo ya sare ya 4-4 kupelekea kupigwa penati na Tanzania ilifungwa kwa penati 4-3 na Msumbiji.
Katika hatua ya pili Tanzania ilishuka dimbani dhidi ya Comoro na kuibuka na ushindi wa 2-1.
Katika mchezo mwingine Tanzania iliibuka na ushidi wa mabao 5-2 dhidi ya Angola.
Kwa upande wa mkuu wa timu ya Taifa ya Ufukweni Boniface Pawasa amesema kuwa kikosi kimejiandaa vyema kwa ajili ya kupata ushindi leo dhidi ya Msumbiji ambao nao ni wazuri.
“Kila timu ni bora kikubwa na kuomba mungu kikosi kucheze kwa maelekezo niliyowafundisha lakini pia nina imani na wachezaji wangu kwani wapo vizuri kuhakikisha wanafanya vyema na kuiwakilisha vyema nchi yao,naomba watanzania waikumbuke timu yao katika maombi ili kuweza kufanya vyema katika mashindano haya”amesema.
Aliongeza kuwa wachezaji wanamorali ya ushindi na wamenihakikishia kufanya vyema katika mchezo huo wa fainali.