Home BUSINESS STAMICO YATOA VIFAA VYA UCHIMBAJI KWA WACHIMBAJI WADOGO WENYE USIKIKIVU HAFIFU

STAMICO YATOA VIFAA VYA UCHIMBAJI KWA WACHIMBAJI WADOGO WENYE USIKIKIVU HAFIFU

Na: Bibiana Ndumbaro, STAMICO.

Katika kusheherekea Maadhimisho ya miaka Sitini ya Uhuru STAMICO  imetoa vifaa vya uchimbaji  kwa Wachimbaji  Wadogo viziwi ambao wameonesha nia ya kujishughulisha na uchimbaji.

Vifaa hivyo vimetolewa Novemba 26, 2021 katika kituo cha mfano kwa Wachimbaji Wadogo kilichopo Lwamgasa  Mkoani Geita, kituo kinachoendeshwa na STAMICO.

Mara baada ya kukabidhi vifaa  vya uchimbaji, Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe.  Wilson Shimo  ameipongeza STAMICO kwa jitahada za kuwasaidia wachimbaji wadogo hususani  kwa kuwakumbuka wachimbaji wa kundi hili maalumu.

Aidha ametoa  shime kwa wachimbaji  wadogo kujiunga katika vikundi ili waweze kupata misaada kwa urahisi zaidi kwa kutumia fursa mbalimbali zinapojitokeza.

“Naamini kwa vifaa hivi  vitawasaidia kuongeza kasi katika uchimbaji  na uzalisha wa Dhahabu. Nimeambiwa vifaa hivi vimegharimu zaidi ya Milion 10 hivyo tunataka kuona uchimbaji wenu unakuwa  bora na wakisasa utakao wasaidia kwemye maisha yenu”, Mhe. Shimo 

Naye Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji, Dkt. Venance Mwasse amesema STAMICO  imeamua kutoa vifaa hivyo ili kuweza kuwashirikisha wachimbaji wadogo katika uchumi jumuishi kupitia shughuli  zao wanazozifanya.

Amewapongeza  wachimbaji hao kwa kuamua kujiishughulisha  katika uchimbaji na kuachana na dhana potofu za kutumia ulemavu kama kinga ya kutokufanya kazi.

Amesema STAMICO  itaendelea kuwa bega kwa bega na wachimbaji hao ili kuona wanaendelea kukua kwa kutumia Tekinolojia ya  kisasa na kuchangia katika  pato la Taifa.

Katika kusheherekea Miaka 60 ya Uhuru  tumeamua kusheherekea miaka 60 kwa kuwapa.

Wachimbaji wadogo wenye usikivu hafifu  msaada wa vifaa vya uchimbaji ambavyo vitawasaidia kwenye kazi zao.  ” Sisi STAMICO tumeamua kuwasaidia nyavu wavue Samaki na sio kuwapa Samaki” Alisema Dr Mwasse.

Aidha, Mwenyekiti wa wachimbaji Wadogo Mkoa Geita Bw. Kadeo,  ametoa rai kwa wachimbaji  waliopatiwa vifaa, kutumia vyema vifaa hivyo kwa manufaa ili viweze kuleta tija kwenye shughuli zao za uchimbaji na  akawasisitiza kutumia masoko ya madini yaliyopo kuuza dhahabu  watakazozipata.

Kwa upande wa Wachimbaji Wadogo Mwenyekiti wa Taasisi ya Viziwi  Tanzania (TAMAVITA) Bw.Nyema  ameishukuru  STAMICO kwa kusaidia  na kuendelea  kuwaamini wachimbaji hawa wenye usikivu  hafifu na kuahidi kuvitumia vifaa hivi kwa umakili ili viweze kuwaletea manufaa.

STAMICO imeendelea kuwasaidia Wachimbaji Wadogo ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kupata dhahabu itayowasaidia kuwaletea maendeleo yao binafsi.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here