Home BUSINESS STAMICO NA BENKI YA KCB WAINGIA MAKUBALIANO KUTOA MIKOPO KWA WACHIMBAJI WADOGO

STAMICO NA BENKI YA KCB WAINGIA MAKUBALIANO KUTOA MIKOPO KWA WACHIMBAJI WADOGO

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Vennance Mwasse (kulia) na Mwakilishi wa Benki ya KCB, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kiislamu wa Benki hiyo (Islamic Banking) Amour Muro (kushoto) wakibadilishana hati za makubaliano mara baada ya kutia saini makubaliano ya mashirikano katika kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo Jijini Dar es Salaam. PICHA NA: HUGHES DUGILO.

Mwanasheria wa Benki ya KCB Antonia Kilama (kushoto) akikamilisha zoezi la utiaji saini kwenye hafla hiyo fupi ya makubaliano hayo yaliyofanyika kwenye Ofisi za STAMICO Jijini dar es Salaam (kulia) ni Mwanasheria wa STAMICO Robert Ambrozi akishuhudia tukio hilo. PICHA NA: HUGHES DUGILO.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Vennance Mwasse (kulia) na Mwakilishi wa Benki ya KCB, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kiislamu wa Benki hiyo (Islamic Banking) Amour Muro (kushoto) wakitia saini hati za makubaliano makubaliano ya mashirikano katika kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo Jijini Dar es Salaam. PICHA NA: HUGHES DUGILO.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Vennance Mwasse (kulia) akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawamo pichani) kabla ya utiaji saini wa Makubaliano hayo. (kushoto) ni Mwakilishi wa Benki ya KCB, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kiislamu wa Benki hiyo (Islamic Banking) Amour Muro. PICHA NA: HUGHES DUGILO.

 

Mwakilishi wa Benki ya KCB, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kiislamu wa Benki hiyo (Islamic Banking) Amour Muro akizungumza kwenye hafla hiyo. PICHA NA: HUGHES DUGILO.


Mwanasheria wa Benki ya KCB Antonia Kilama (kulia) akiwa na Afisa mwenzake wa Benki hiyo wakifuatia hotuba ya Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kiislamu wa Benki hiyo (Islamic Banking) Amour Muro (hayumo pichani) wakati wa hafla hiyo. PICHA NA: HUGHES DUGILO.

Wanasheria kutoka STAMICO na Benki ya KCB, Robert Ambrozi (wa kwanza kulia) na Antonia Kilama (wa kwanza kushoto) wakishuhudia makabidhiano ya hati za makubaliano kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Vennance Mwasse (wa pili kulia) na Mwakilishi wa Benki ya KCB, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kiislamu wa Benki hiyo (Islamic Banking) Amour Muro (wa pili kushoto) mara baada ya kumalizika zoezi la utiaji saini wa hati hizo katika Ofisi za STAMICO Dar es Salaam. PICHA NA: HUGHES DUGILO.
Maafisa wa Benki ya KCB na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa zoezi hilo. PICHA NA: HUGHES DUGILO.

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Benki ya KCB wameingia makubaliano yanayolenga kushirikiana katika kutoa mikopo ya kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata mikopo endelevu na kwa rahisi zaidi ili  waweze kufanya shughuli za uchimbaji zenye tija.

 

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya kusaini Hati ya makubaliano (MOU) baina ya pande hizo mbili leo Novemba 16, 2021 katika Ofisi za STAMICO Jijini Dar es Salaam. 

 

Akizungumza wakati wa utiaji saiini Makubaliano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Vennance Mwasse amesema kuwa Malengo ya makubaliano hayo ni kushirikiana na Taasisi za fedha katika kuwasaidia wachimbaji wadogo kupata mikopo endelevu na yenye tija.

 

“Katika Makubaliano haya STAMICO itawajibika kutoa utaalam elekezi katika maeneo ya Jiolojia, Uchimbaji na Uchenjuaji Madini kwa miradi ya Wachimbaji Wadogo ambayo itafanya maombi ya mikopo na kuiwasilisha kwa Benki kabla ya utekelezaji wake na Benki ya KCB itawajibika kutoa mikopo kwa Wachimbaji Wadogo ambao watawasilisha maombi ya mikopo katika maeneo ya miradi ya uchimbaji madini itakayokidhi vigezo vya kupewa mikopo.Amesema Dkt. Mwasse.

 

Ameongeza kuwa Makubaliano hayo yatadumu kwa muda wa miaka mitatu (3) kuanzia mwaka huu wa 2021 ambapo pia yanaweza kufanyiwa mapitio kila baada ya mwaka mmoja (1).

 

Kwa upande wake Mwakilishi wa Benki ya KCB, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kiislamu (Islamic Banking) Amour Muro amesema kuwa Benki hiyo imekuwa ikitoa Huduma ya mikopo mbalimbali isiyokuwa na riba nakwamba wachimbaji wadogo wanakaribishwa kupata mikopo hiyo hata kwa wale ambao sio waislamu.

 

“Mpaka sasa Benki yetu tayari imeshatoa mikopo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 4 kwa wateja wetu wote na sasa tupo tayari kuwafikia wachimbaji wadogo kwa kuwakopesa ili waweze kufanya shughuli zao” Amesema Amour.

 

STAMICO imendelea kutekeleza mikakati yake ya kuendeleza shughuli za uchimbaji mdogo nchini ili uwe wenye tija na kuchangia ipasavyo uchumi wa nchi ikiwa ndio Mlezi wa Wachimbaji Wadogo hapa nchini.



Previous articleHABARI ZILIZOPO MAGAZETI YA LEO J.NNE NOVEMBA 16-2021
Next articleUHUSIANO WA KIMATAIFA NI KIPAUMBELE CHA RAIS SAMIA – MAJALIWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here