Home SPORTS SIMBA YAICHAPA RED ARROWS TATU MZUKA

SIMBA YAICHAPA RED ARROWS TATU MZUKA



Na: Stella  Kessy, DAR ES SALAAM.

MABINGWA wa ligi kuu Tanzania bara Simba leo wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Red Arrows kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Katika mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90, Kocha Mkuu, Pablo Franco hakuwa na namna ya kufanya kutokana na mazingira ya uwanja kutokuwa rafiki kwa kuwa uwanja ulikuwa na maji baada ya mvua kunyesha ila hiyo haikuwa tatizo ushindi ulipatikana.

Hata hivyo katika mchezo wa leo kiungo mshambuliaji, Bernard Morrison ameonyesha makeke yake na kuhusika katika upatikanaji wa mabao yote matatu ambayo yalifungwa ndani ya dakika 90.

kiungo huyo mshambuliaji Morrison alitupia mabao mawili ilikuwa dakika ya 16 na dakika ya 77 huku moja lilifungwa na Meddie Kagere dakika 19 kwa pasi ya Morrison.

Mpaka dakika 90 zinakamilika  simba alifanikiwa kuongoza kwa bao 3 -0 dhidi ya wapinzani wao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here