Home SPORTS SIMBA WAINGIA KAMBINI LEO

SIMBA WAINGIA KAMBINI LEO

 

 Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

MABINGWA watetezi wa ligi kuu  Simba leo kimeingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Ruvu Shooting  utakaochezwa Novemba 19 katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Hata hivyo kikosi hicho kiliendelea na mazoezi ambapo wachezaji walikuwa wanatokea nyumbani ila kwa leo jioni wataingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mtanange huo.

Pia wachezaji ambao walikuwa katika timu ya taifa ya Stars wataungana na wenzao leo kambini.

Nyota wa kikosi hicho watatu Rally Bwalya, Duncan Nyoni, na Peter Banda wao hawataingia kambini leo kutokana na kuwa na majukumu ya timu yao zao za taifa na wanatarajiwa kutua nchini baada ya kumaliza mechi zao.

Hata hivyo itakuwa kambi ya kwanza kwa kocha Mkuu Pablo Franco ambaye ametua nchini siku tano zilizopita tayari kukinoa kikosi chetu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here