Home LOCAL SERIKALI WAIPONGEZA SHULE YA BRIGHT AFRIKAN

SERIKALI WAIPONGEZA SHULE YA BRIGHT AFRIKAN

Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira Othiman Chande akizungumza na Wazazi na Wanafunzi wa Shule ya Bright Afrika Iliyopo Kivule Wilaya Ilala (Kulia)Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa na Mkurugenzi wa Shule ya Bright Afrika Wiliam Komba Picha na Heri Shaaban.

Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira Othiman Chande akizungumza na Wazazi na Wanafunzi wa Shule ya Bright Afrika Iliyopo Kivule Wilaya Ilala (Kushoto)Mkurugenzi wa Shule ya Bright Afrika Wiliam Komba Picha na Heri Shaaban.


Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jery Silaa akipanda miti kwa ajili ya utuzaji wa Mazingira shule ya Bright Afrika iliyopo Kivule Wilayani Ilala Novemba 20/2021(Kushoto )Mwenyekiti wa Mtaa wa Kivule Amos Hangay (Picha na Heri Shaaban)

Diwani wa Kata ya Mzinga Job Isack akipanda mti katika Shule ya Bright Afrikan Iliyopo Kivule Wilayani Ilala Novemba 20/2021.(Picha na Heri Shaaban).

Na:Heri Shaaban

SERIKALI wameipongeza shule ya Bright Afrikan kwa upandaji miti na  uzunzaji mazingira ya    shule yao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Othiman Chande katika harambe ya utunzaji Mazingira  ya Shule ya Bright Afrikan  iliyopo Kivule Wilayani Ilala .

“Naipongeza shule yenu Bright Afrikan    kwa mazingira mazuri ya upandaji miti na utunzaji mazingira Ujumbe wa Mazingira ” Tunza Mazingira ishi kwa furaha bila taaruki “alisema Othiman.

Naibu Waziri Othiman alisema ni muhimu kutunza mazingira kwa ajili ya kutunza vyanzo vya maji  ,maji yana kazi kubwa kwa jamii na Taifa kwa ujumla .

Aliziagiza shule zote kupanda miti nchini kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji kwani yana faida kubwa viwanda vinategemea na umeme .

Akizungumzia shule hiyo amemwagiza Mkurugenzi wa shule kukuza lugha ya Kiswahili na Taaluma   kwa ajili ya kuongeza ufaulu masomo yao

Aliwataka wazazi, Walimu na Wanafunzi kushirikiana na kuwekeza katika sekta ya elimu.

Kwa upande wake Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa alisema Barabara zote za Jimbo la Ukonga zimekabidhiwa Wakandarasi ujenzi utaanza hivi karibuni .

Mkurugenzi wa Shule ya Bright Afrikan  Wiliam Komba shule hiyo ilianza mwaka 2016  shule hiyo ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri katika mitihani ya Kitaifa mwaka 2021 ngazi ya Taifa matokeo ya darasa la saba imekuwa shule ya 34 Kati ya shule 11,909.

Komba alisema  mikakati waliojiwekea utunzaji wa mazingira kwa faida ya Taifa lengo la shule hiyo kupanda miti ya matunda na kusambaza kwa jamii.

Katika harambee shuleni hapo Naibu Waziri Mazingira na Muungano Othiman Chande alichangia milioni mbili na mifuko 30  ya cementi Mbunge wa Ukonga Jery Silaa alichangia milioni 2 Diwani wa Mzinga Job Isack shilingi 150,000/=Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kivule Amos Hangaya pia alichangia shilingi 100,000/= kwa ajili ya mazingira.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here