Home LOCAL RC SINGIDA AKABIDHI BASI HOSPITALI YA MANDEWA KWA AJILI YA KUSAFIRISHIA WAFANYAKAZI

RC SINGIDA AKABIDHI BASI HOSPITALI YA MANDEWA KWA AJILI YA KUSAFIRISHIA WAFANYAKAZI

Basi namba STL 9908 lililokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge kwa ajili ya wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida

Na: Mwandishi Wetu, Singida.

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amezindua Rasmi  na kukabidhi basi aina ya Coaster kwa ajili ya kusafirishia wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mandewa iliyopo mkoani hapo kama kitendea kazi kitakachowasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

Akizungumza na wafanyakazi akiwa Hospitalini hapo baada ya kuwakabidhi basi Mkuu wa Mkoa amewapongeza watumishi kwa namna ambavyo wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu  na wengi wao wakitumia bodaboda kufika kazini lakini pia hawakukata tamaa.

RC Mahenge amemtaka Afisa usafirishaji wa Hospitali ya Mkoa wa Singida kuhakikisha basi hilo linatunzwa na kuzingatia muda wa  kufanyia huduma (service) kila inapofika muda wake ili kulifanya lidumu kwa muda mrefu na kuendelea kuwasaidia watumishi.

Amewataka madaktari katika hospitahi hiyo ambayo ni Tawi la Hospitali ya Mkoa wa Singida  kuboresha huduma zao na kuzifanya ziwe za kibingwa  ili kuifanya Singida kuwa kimbilio la  mikoa ya jirani (center of excellence )

Aidha ameitaka bodi ya Hospitali hiyo kuanza kufikiria namna ya kujenga nyumba za watumishi kupitia vyanzo vyao vya ndani au kupitia  mashirika mbalimbali  kwa kuwa kukaa karibu na hospitali kunaongeza ufanisi katika kazi.

Akimalizia hotuba yake mkuu wa mkoa amewataka madaktari hao pamoja na bodi kuyafanya majengo ya zamani kuwa hospitali ya Wilaya halafu majengo ya Hospitali ya Mandewa yatumike kama hospitali ya mkoa.

Awali Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa  Dkt. Deogratius Banuba akisoma hotuba yake alisema gari hilo lina thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 236 ambazo zilitokana na makusanyo ya ndani.

Hata hivyo amemhakikishi RC kwamba gari hilo litatumika kubeba watumishi kuwaleta kazini na kuwarudisha na pia kutumika katika shughuli za kijamii kwa watumishi 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here