Home SPORTS RAIS SAMIA ATOA MILIONI 150 “TEMBO WARRIORS”

RAIS SAMIA ATOA MILIONI 150 “TEMBO WARRIORS”




Na: Mwandishi wetu

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, leo, ametembelea kambi na mazoezi ya Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu kwa wenye ulemavu, Tembo Warriors, wanaoendelea na maandalizi ya kufuzu Kombe la Dunia kupitia michuano ya Afrika (Canaf) inayofanyika Dar es Salaam, Tanzania.

Katika matembezi hayo waziri alikuwa ameambatana na Mawaziri wa Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Jenister Mhagama, Katibu Mkuu wa Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu-Ofisi ya Waziri Mkuu, Tixon Nzunda, na viongozi wengine wa Serikali, Waziri Mkuu Majaliwa ametoa salaam za Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na motisha ya Rais kwa timu hiyo.

“Mhe Rais anafahamu mko hapa mnajiandaa kuipigania nchi na amesema nije hapa kwa niaba yake na ametoa kiasi cha Shilingi milioni 150 kuhakikisha ninyi na timu zote za Afrika zinazokuja Tanzania zinakaa hapa vizuri,” alisema Mhe. Majaliwa. 

Tanzania ni mwenyeji wa mashindano hayo ambapo timu kutoka nchi 15 zinashiriki kwa ukanda wa Afrika ambapo timu nne zitafuzu kwenda mashindano ya dunia.

Previous articleSERIKALI HAITAVUMILIA VITENDO VYA UKATILI WOWOTE WA KIJINSIA – MAJALIWA
Next articleMKUU WA WILAYA TANDAHIMBA AIPONGEZA REA KWA KAZI NZURI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here