Home LOCAL PROF. MAKUBI AISIFU SEKOE TOURE KWA KUANZISHA KAMBI ZA HUDUMA ZA UCHUNGUZI...

PROF. MAKUBI AISIFU SEKOE TOURE KWA KUANZISHA KAMBI ZA HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA KIBINGWA



Na:WAMJW-MWANZA.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ameupongeza uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure iliyoko jijini Mwanza kwa kuanzisha makambi ya huduma za kibingwa za uchunguzi bila malipo.

Prof. Makubi ametoa pongezi hizo leo wakati alipotembelea katika Hospitali hiyo kwa lengo la kuangalia namna huduma za afya zinavyotolewa sambamba na maboresho ya huduma za uchunguzi, ujenzi wa sehemu ya kufua hewa ya oksijeni na kuangalia maendeleo ya jengo la mama na mtoto pamoja na utekelezaji wa miradi ya fedha za IMF.

Kufuatia hatua hiyo Prof. Makubi ametoa wito kwa vituo vya afya nchini kuanzia Hospitali za ngazi ya taifa hadi wilaya kuwa na utaratibu wa kuweka kambi za bure kwa wananchi walau kila baada ya miezi miwili kwa ajili ya uchunguzi wa kibingwa wa magonjwa hasa yasiyokua ya kuambukiza na kuwasisitiza wananchi kujitokeza kupima afya zao.

Kuhusu fedha za IMF Prof. Makubi amesema Hospitali ya Sekoue Toure imetengewa zaidi ya shilingi bilioni 1.9 kwa ajili ya vifaa vitakavyonunuliwa na kufungwa katika jengo la mama na mtoto  ambalo linatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 22 mwaka huu na kuanza kutoa huduma kabla mwaka huu 2021 haujaisha.

Aidha, Prof Makubi ameendelea kusisitiza viongozi wote wa vituo vya afya nchini  kusimamia vyema matumizi ya fedha katika ujenzi na ununuzi wa vifaa kwa kushindanisha wazabuni na wakandarasi ili thamani ya fedha iweze kuonekana huku akitoa miezi saba kuanzia tarehe 22 Novemba mwaka huu miradi yote iwe imeanza na kukamilika hadi kufikia tarehe 30 June mwaka 2022.

Previous articleSERIKALI YA MAREKANI KUTOA 437 KWAAJILI YA MIRADI YA AFYA.
Next articleHABARI ZILIZOPO MAGAZETI YA LEO J.NNE NOVEMBA 16-2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here