Home Uncategorized PAWASA: WATANZANIA ENDELEENI KUIOMBEA DUA TIMU YENU

PAWASA: WATANZANIA ENDELEENI KUIOMBEA DUA TIMU YENU

Na: Stella Kessy.

KOCHA  Mkuu wa Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni Boniface Pawasa amewataka Watanzania kuzidi kuiombea timu leo inashuka dimbani  dhidi ya Angola katika  mashindano ya COSAFA yanayofanyika Durban, Afrika Kusini.

“Mimi ninaomba watanzania wazidi kutuombea kwani maombi ndio kitu kizuri licha ya kuwa tumejipanga vizuri tunaenda kucheza na timu  ngumu, pia  na sisi tumejipanga kuitangaza vyema nchi yetu katika mashindano haya ambayo kila timu imejipanga vyema kuhakikisha wanafanya vyema”amesema.

Amesema kuwa timu zote zinazokutana ni ngumu hivyo hakuna budi kufanya vyema katika mchezo huo kwani wamejipanga vyema kuhakikisha timu inaibuka na ushindi.

Kikosi hicho kinashuka leo dimbani  dhidi ya Angola ambao jana walishinda bao 8 -6 dhidi ya Afrika kusini huku Tanzania wao walishinda bao 2-1 dhidi ya  Comoro.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here