Home SPORTS PAWASA: TUTAWAKILISHA VYEMA MICHUANO YA BEACH SOCCER

PAWASA: TUTAWAKILISHA VYEMA MICHUANO YA BEACH SOCCER

 

Na: Stella kessy.

Jumla ya wachezaji 14 wameondoka alfajiri ya leo kwa ajili ya kuondoka  michuano ya Afrika ya Beach  Soccer yanayafanyika huko afrika kusini Septemba 17   mwezi huu.

Akizungumza jana wakati wanaanza safari  kocha mkuu kwa timu hiyo, Boniface pawasa amesema kuwa kikosi kimejiandaa vya kutosha kwa ajili ya kupata ushindi katika michuano hiyo.

Amesema kuwa maandalizi yamefanyika vyema kwa lengo la kufanya vyema na kupeperusha bendera ya Tanzania vyema.

Ameongeza kuwa kikosi kina morali ya ushindi kwani wachezaji wenyeji wapo saba na wageni wapo 7 ambapo kikosi kina hali ya ushindani na wamelenga kufanya vyema katika michuano hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here