Home SPORTS PABLO AONGOZA MAZOEZI YA SIMBA KWA MKAPA

PABLO AONGOZA MAZOEZI YA SIMBA KWA MKAPA

 

 Na: Stella kessy

KOCHA Mkuu wa kikosi cha mabingwa Simba Pablo  Franco, leo ameongoza mazoezi kwa mara ya kwanza kwa kikosi chake katika Uwanja wa Mkapa.

Kikosi cha simba kina kibarua kigumu kwa ajili ya  mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao ni wa mtoano na unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Hata hivyo katika mchezo huo ambao jana wametangaza kuingiza mashabiki 35,000 kwa jili ya kucheki mchezo huo.

Kwa Mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba (C.E.O), Barbara Gonzalez amesema kuwa kikosi kimejiandaa vyema  katika mchezo huo dhidi ya Red Arrow.

“Hii ni mechi ya pili lakini pia ni mechi ya kwanza inayochezwa katika dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam,sina shaka na kocha pamoja na wachezjai nina imani kikosi kipo vyema hata katika maandalizi tumeona wachezaji wana morali ya ushindi  kikubwa ni kuwaombea wachezaji ili kuweza kufanyia kazi mafundisho ya waliofundishwa na kocha” amesema.

Ameongeza kuwa katika klabu ya simba viongozi wanatambua umuhimu wa mechi hii na malengo yetu ni kuhakikisha kikosi kinaingia katika hatua ya makundi.

Amesema kuwa katika michuano hiyo ambayo nguvu imewekwa ya kutosha kama ilivyokuwa katika michuano ya klabu bingwa hivyo klabu pamoja na viongozi hawana shaka na uwekezaji katika klabu.

Pia amefafanua kuwa katika suala la kukata tiketi bei zimeshatajwa tangu juzi kikubwa tunawaomba wadau na wapenzi wa simba kuzidi kujitokeza kwa wingi ili kuongeza hamasa kwa wachezaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here