Home SPORTS NAMUNGO FC YACHEZEA KICHAPO 3-1 MBELE YA PRISONS

NAMUNGO FC YACHEZEA KICHAPO 3-1 MBELE YA PRISONS

Na: Mwandishi wetu, SUMBAWANA.

KIKOSI cha Tanzania Prisons leo kimeibuka na ushindi  baada ya kuichapa Namungo 3-1  katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.

Mabao yote ya Tanzania Prisons  yamefungwa na mshambuliaji Jeremiah Juma dakika ya nne, 11 na 26, wakati bao pekee la Namungo FC limefungwa na mshambuliaji Mrundi, Bigirimana Blaise dakika ya 68.

Hata hivyo katika  ushindi huo, Prisons inafikisha pointi nane na kujiinua hadi nafasi ya nane, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake sita katika nafasi ya 13 baada ya wote kucheza mechi 13.

Mtanange mwingine ulikuwa kati ya Mbeya City na KMC  ambao wametoka sare kwa bao 2-2

Katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Huku mabao ya Mbeya City yamefungwa na Paul Nonga dakika ya nane na Richardson Ng’ondya dakika ya 67 na ya KMC yamefungwa na Matheo Anthonyu dakika ya 13 na Mohamed Samatta dakika ya 86.

Kwa matokeo hayo, Mbeya City inafikisha pointi 11 na kusogea nafasi ya tatu, wakati KMC inafikisha pointi sita na inabaki nafasi ya 14 kwenye ligi ya 16 baada ya timu zote kucheza mechi saba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here