Home SPORTS MNYAMA VITANI LEO KUTETEA NCHI

MNYAMA VITANI LEO KUTETEA NCHI

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

MABINGWA wa ligi kuu Tanzania bara Simba leo wanashuka dimbani kuchuana na Red Arrows Katika michuano ya Kombe la shirikisho Afrika  utakaochezwa katika  dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha simba kinaingia uwanjani kwa machungu na tahadhari kubwa baada ya kuondolewa  katika mashindano ya ligi ya mabingwa Afrika kwa kupoteza mchezo wake dhidi Galaxy kwa kipigo cha 3-1 kiwa nyumbani.

Kikosi hicho kipo chini ya kocha mkuu Pablo Franco, ambaye ni mechi yake ya kwanza ya  kimataifa huku ni mchezo wake wa pili akiwa na kikosi hicho.

Kocha huyo amesema kuwa kikosi chake kina malengo ya kuhakikisha wanafanya vyema katika mchezo huo na kuwatoa  wapinzani wao katika mashindano  kutokana na maandalizi makubwa waliofanya tangu yeye kuingia katika kikosi hicho.

Pablo ametoa kauli hiyo kuelekea mchezo wa kwanza wa kimataifa tangu ajiunge na timu hiyo, akichukua mikoba ya Didier Gomes Da Rosa, ambaye aliachia ngazi baada ya kufanya vibaya kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pablo amesema kuwa anachokiangalia kwa sasa ni kuona wanafanikiwa kupita kwenye hatua hiyo kwenda makundi kwa kuwa ni  malengo waliopanga.

“Tunaenda kwenye mchezo mgumu lakini matarajio yetu ni kupata matokeo mazuri kutokana na maandalizi ambayo tumekuwa tukiendelea nayo kabla ya kuelekea Zambia katika mchezo wa marudiano. 

“Wapinzani wetu siyo wabaya na tunapaswa kuwaheshimu lakini kitu kikubwa ambacho tunakiangalia ni kwa jinsi gani tunaweza kutengeneza matokeo makubwa hapa ili iwe rahisi kwetu kufuzu kwenda katika hatua ya makundi, jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wetu,” amesema Pablo.

Kwa upande wake Nahodha wa timu John Bocco amesema maandalizi ya kuelekea katika mchezo huo ni mazuri kwani wamejipanga kuhakikisha wanapata matokeo.

Amesema kuwa watakikisha wanafanya vyema kwani kutolewa katika michuano ya klabu bingwa yaliwaumiza sana kwa sasa hawapo tayari kirudia makosa.

“Kama kikosi pamoja na benchi zima la ufundi tumeiangalia Red Arrows kupitia mkanda wa video i timu nzuri na tunajua nao wamejipanga na wametufuatilia lakini lakini tumejidhatiti kuhakikisha simba inaingia katika hatua ya makundi katika michuano ya shirikisho”amesema.

amesema kuwa wachezaji wamejipanga kuhakikisha wanapata matokeo licha ya wapinzani wao kuwa wazuri lakini wamelenga kupambana ili kupata matokeo.

Previous articleMAGAZETI YA LEO J.PILI NOVEMBA 28-2021
Next articleJENERALI IBUGE AWAPONGEZA WANANCHI WA KIJIJI CHA RUANDA KWA KUCHANGIA MAENDELEO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here