Home LOCAL MKURUGENZI WA SEKONDARI YA MARSHI NA DIWANI MATIKO KIZIMBANI KWA ‘KUCHAKACHUA’ SH....

MKURUGENZI WA SEKONDARI YA MARSHI NA DIWANI MATIKO KIZIMBANI KWA ‘KUCHAKACHUA’ SH. MILIONI 80.4



Diwani wa Kata ya Nyarukoba, Halmashauri ya Tarime mkoani Mara, Juma Athuman Matiko (aliyejificha sura kwa shati lenye rangi ya Zambarau), akipelekwa kwenye gari tayari kwenda mahabusu, baada ya kusomewa shitaka la kugushi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma.

Na: Mwandishi Wetu, Musoma.

MKURUGENZI wa Sekondari ya Marshi ya mjini Musoma, Denis Karume Nyakira na Diwani wa Kata ya Nyarukoba Halmashauri ya Tarime mkoani Mara, Juma Athuman Matiko (35) wanashitakiwa kwa uhujumu uchumi.

Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wiliam Lyamboko akishirikiana na Wakili wa Serikali Marshal  Mseja, wamesoma kesi hiyo namba  25 ya Mwaka 2021 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma, Eugenia Rujwahukseja.

Ameieleza Mahakama kuwa Mshitakiwa wa kwanza Mwaka 2015, Nyakira alifanya ubadhilifu wa Sh. Milioni 80.4 kinyume na kifungu cha 28 (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Kwamba huku akifahamu kuwa Mgodi wa North Mara  ulikuwa unalipia ada wanafunzi 34, alipokea ada ya wanafunzi 134 kupitia akauti ya benki ya shule hiyo na akazitumia zote ilhali akifahamu kuwa Sh. Milioni 80.4 ilikuwa imezidiyozidi malipo halali.

Kwa upande wa mshtakiwa wa Pili, Mseja ameieleza mahakama kwamba akiwa kiunganishi kati ya wanakijiji cha Genkuru kilichopo Kata ya Nyarukoba na Mgodi wa North Mara aligushi orodha ya majina ya wanafunzi akionesha waliotakiwa kulipiwa ada walikuwa 134. Upelelezi wa kesi hiyo umekamilika. 

Kuhusu dhamana kwa washitakuwa hao, Mseja amepinga lililowasilishwa na Wakili  wa washitakiwa, Amosi Wilison, kwamba licha ya kibali cha Mwendesha mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) kwa mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo, kisheria haina mamlaka ya kuamua juu ya dhamana ya washtakiwa hao, ombi inatakiwa lipelekwe Mahakama Kuu.

Naye Wilson ameomba mahakama kurejea hati ya mashtaka kwamba kila mshtakiwa anakabiliwa na shitaka lake.

Kwamba Matiko inawezekana kudhaminiwa,katika mahakama hiyo kwasababu anashtakiwa kwa kugushi tofauti na Nyankira anayeshitakiwa kwa ubadhilifu wa  lake zaidi ya Sh. Milioni 10.

Hakimu Rujwahuka amekubali Matiko adhaminiwe na wadhamini wawili wenye vitambulisho vya taifa pamoja na makazi ya kudumu yaliyo ndani ya Mkoa huo, yenye hati miliki.

Mmoja kati ya wadhamini hao hakukamilisha sharti la kuwa na hati ya makazi hivyo washitakiwa wote wamepelekwa mahabusu mpaka Novemba 23 Mwaka huu, kesi itajwa tena kwa ajili ya kuwasomea mashitaka ya awali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here