Home SPORTS MHE. BASHUNGWA ATAKA MICHEZO YA WENYE ULEMAVU KUWA MICHEZO YA KIPAUMBELE

MHE. BASHUNGWA ATAKA MICHEZO YA WENYE ULEMAVU KUWA MICHEZO YA KIPAUMBELE






Na: John Mapepele, WUSM

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa amewaagiza Watendaji Wote, wa Sekta ya michezo kuhakikisha michezo ya wenye ulemavu, hususan soka kuwa miongoni mwa  michezo ya kipaumbele na kuitaka kuingizwa kwenye mifumo rasmi, ya kukuza vipaji, kama UMITASHUMTA na UMISSETA.

Mhe. Bashungwa ameyasema hayo leo Novemba 27, 2021 wakati alipokuwa akifungua mashindano ya Afrika ya Mpira wa Miguu kwa watu Wenye ulemavu kwa wanaume (CANAF 2021) katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

“Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatambua thamani na fursa zilizopo katika michezo yote, ikiwemo kundi la watu wenye ulemavu. Kwa msingi huo tumechukua jukumu hili, ili kuhakikisha fursa hii inatumika vema kuiweka timu yetu ya soka ya Taifa kwa walemavu, ya Tembo katika ramani ya mchezo huu kimataifa”. Amefafanua Mhe Bashunga
Akimkaribisha kufungua mashindano hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt. Ally Possi amesema Tanzania inathamini watu wenye ulemavu ndiyo maana imeendelea kuratibu mashindano haya baada ya yale ya awali ya mashindano ya ulimbwende ya Miss na Mr Afrika kwa viziwi kwa Bara la Afrika yaliyoisha hivi karibuni.

Aidha, amesema Serikali baada ya kupitisha bajeti ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa itaendelea kutenga fedha mahususi kwa ajili ya michezo ya watu wenye ulemavu.Rais wa Shirikisho la mchezo wa Soka kwa watu wenye ulemavu nchini Peter Sarungi amesema mashindano ya mwaka huu yamevunja rekodi  kwa kuwa na  washiriki wengi ambapo pia amemshukuru Rais kwa kusaidia michezo ikiwa ni pamoja na wenye ulemavu.

 Mkurugenzi wa Michezo nchini ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya michezo hiyo hapa nchini Yusufu Omary Singo amesema serikali itaendelea kusimamia michezo yote kikamilifu ikiwa ni pamoja na michezo ya wenye ulemavu.

Previous articleTMDA YATOA TATHIMINI YA UTEKELEZAJI WA MWAKA MMOJA WA MRADI WA ASCEND
Next articleMHE. BASHUNGWA AFUNGUA RASMI MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU KWA WENYE ULEMAVU (Canaf)
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here