Home SPORTS MHE. BASHUNGWA AFUNGUA RASMI MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU KWA WENYE ULEMAVU...

MHE. BASHUNGWA AFUNGUA RASMI MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU KWA WENYE ULEMAVU (Canaf)

 

Na: Stella Kessy.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa   leo amefungua mashindano ya mpira wa miguu kwa mataifa Afrika kwa watu wenye ulemavu (Canaf) yanayofanyika Dar es Salaam, Tanzania.

Katika mashindano hayo jumla ya nchi 14 zinashiriki huku nchi zilizowasili hadi sasa ni 13 huku washiriki wengine timu ya taifa ya Nigeria inatarajiwa kuwasili leo usiku.

Tanzania ni mwenyeji wa mashindano hayo ambapo timu kutoka nchi 14 zinashiriki kwa ukanda wa Afrika ambapo timu nne zitafuzu kwenda mashindano ya dunia.

Amesema kuwa lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuzidi kuinua michezo katika sekta mbalimbali hapa nchini.

“Ninachoomba walemavu watambue kuwa rais anatambua thamani ya michezo hapa nchini hivyo ni vyema wajitahidi kufanya vyema ili kuweza kuongeza hamasa kwa uongozi” amesema

Huku amewataka watu wenye ulemavu kutumia fursa za michezo vizuri kwa kufanya vyema katika michuano hii ili kuinua michezo hapa nchini.

Ameongeza kuwa lengo la  mashindano haya ni kwaajili ya kujenga utimamu na akili kwa  walemavu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here