Home LOCAL MEYA KUMBILAMOTO VINGUNGUTI YATOA MIKOPO YA SERIKALI JUMLA YA SHILLINGI 914,260,000

MEYA KUMBILAMOTO VINGUNGUTI YATOA MIKOPO YA SERIKALI JUMLA YA SHILLINGI 914,260,000

NA:  HERI SHAABAN.

MEYA wa Halmashauri ya Dar es salaam Omary Kumbilamoto amesema Kata ya Vingunguti iliyopo Wilayani Ilala imenufaika na mikopo ya asilimia 10 kutoka Halmashauri ya Jiji ambayo inatolewa na SERIKALI kupitia Halmashauri ambapo Jumla ya shilingi 914,260,000 zatolewa kwa vikundi.

Meya Kumbilamoto alisema hayo Dar es salaam Jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika sokoni kwa Simba ambapo alisema mikopo hiyo ni asilimia 4 ya vijana asilimia 4 ya wanawake na asilimia 2 watu wenye Ulemavu .

Alisema Kata ya Vingunguti vikundi 73 wamenufaika Jumla ya shilingi 914,260,000  ambapo Jumla ya vikundi vilivyochukua mikopo hiyo ya Serikali vikundi vya vijana 32 ,Vikundi vya wanawake 36 na vikundi vitano vya watu wenye Ulemavu

Meya Kumbilamoto alivitaja baadhi ya vikundi vilivyowezeshwa fedha hizo za Halmashauri Mtaa Kombo ,Umoja ni Nguvu,Ujasiliama Family,Famasa Group,Upendo Group,Mzige,Hatushindwi Group, Nyuki,Tubadilike ,Jipe Moyo, Chakale,

Mtaa Majengo Kikundi cha Dunduliza hapa kazi tuu,mchakamchaka,Wazalendo halisi,Maendeleo Women ,Mtaa wa Mtambani Twejune,Umoja,Upendo,Buldoza Umoja wa wauza Karanga,Mtambani youth,kwa Samba Group ,Umoja wa wajasiriamali,VINGUNGUTI group na kazi group.

Alisema mikopo hiyo  anasimamia katika utekelezaji wa ILANI ya CCM  wananchi wake wajikwamue kiuchumi  wakuze mitaji yao inatolewa na SERIKALI aina riba yoyote vikundi vyote vya Kata Vingunguti vinapewa ushirikiano na Ofisi ya Diwani na Afisa Maendeleo wa Kata kwa ushirikiano mkubwa.

Meya Kumbilamoto aliwataka wakope mikopo hiyo na kurejesha kwa wakati ili wengine waweze kukukopa.

Akizungumzia maji safi na Salama Vingunguti upatikanaji wa maji safi na Salama ya DAWASA unaendelea kuimalika Serikali kupitia DAWASA inaendelea kuboresha na kusambaza miundombinu ya maji na visima vya watu binafsi .

Kwa upande wa Sekta ya Ustawi wa Jamii alisema mashauri ya ndoa yamepokelewa 15 watoto waliozaliwa nje ya ndoa 28 ,kesi tatu za Ukatili wa Kijinsia zilizopokelewa watoto watatu wa mitaani wamepelekwa katika Kituo cha kulea watoto ,na watoto watatu yatima wamepelekwa shule ya wadau Cotolengo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki .

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here