Meya wa Jiji la Arusha Maxmillan Iranqe akizindua Taasisi ya Compassion Alumni kwa kushirikiana na Diwani wa kata ya Ngarenaro Issaya Doita, wengine Ni viongozi wa tasisi hiyo.
Diwani wa kata ya Ngarenaro Issaya Doita akishirikiana na watoto wanaofadhiliwa na Compassion Tanzania kukata keki ya kuzindua taasisi ya Compassion Alumni.
Faraja Fredrick mmoja wa wakurugenzi wa tasisi hiyo hasa kituo namba 200 akielezea dhima ya kuanzishwa kwa umoja huo.
Meya wa jiji la Arusha Maxmillan Iranqe amewataka vijana kujiwekea mipango itayowasaidia kutengeneza ajira zao binafsi na kuweza kufikia malengo yao lakini pia kuajiri vijana wengine Kama vile kuanzisha viwanda vidogo vidogo badala ya kusubiri kuajiriwa.
Meya huyo aliyasema hayo wakati akizindua Taasisi ya Compassion Alumni Tanzania tasisi iliyoanzishwa na vijana wanufaika wa ufadhili wa Compassion katika masomo yao ambapo alisema kuwa vijana wakijiwekea mipango ya namna ambavyo wanatama kuwa itasaidia wao kutengeneza ajira zao na kuajiri wengine jambo ambalo litapunguza changamoto ya ajira nchini.
“Wekeni akili zenu kwenye malengo yenu kama mnatamani kufanikiwa, msiridhike na vile vidogo mlivyonanvyo bali angalieni malengo yenu na kuanza kufanya kazi lakini pia muwe na deadline jipangieni muda wa kufanya jambo na kutekeleza kwa wakati sio unaweka malengo miaka na miaka na hakuna maendeleo yoyote,”Alisema Meya Maxmillan.
Alisema kuwa katika kutafuta mafanikio ni vema pia vijana wakachagua aina ya marafiki aina ya marafiki wanaofuatana nao kwa umakini mkubwa ambapo aliwasihi kuchagua marafiki waliofanikiwa na wanaojielewa.
“Chagueni marafiki kwa umakini lakini pia nendeni mkatengeneze ajira kwa namna hiyo mtaitengeneza Tanzania nzuri zaidi yenye mafanikio katika uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla,” Alisema.
Akisoma risala ya vijana wa Taasisi ya Compassion Alumni Tanzania rais wa taasisi hiyo Eric Mramira alisema kuwa lengo la kuunda umoja huo ni kurudisha fadhila kwa jamii ili jamii iweze kunufaika na walichokipanda kwao kwa kuboresha maisha ya watoto kupitia elimu, michango na uwakili.
“Pia kupitia umoja huu tutakuwa na mradi wa ufadhili ili kufikia jamii kubwa zaidi lakini pia tutashirikiana na makanisa ya kiinjili katika programu za ushauri kwa vijana pamoja na kuibua fursa za kiuchumi kwa kubuni miradi itakayowawezesha Alumni kujikwamua kiuchumi,” Alisema Mramira.
Alifafanua kuwa umoja huo umeanzishwa mwaka 2012 na Hadi sasa wamefanikiwa kutoa misaada mbalimbali kwa jamii kwa kusaidia vijana waliokwama kitaaluma kwenye shule mbalimbali za mkoa wa Arusha, kutembelea vituo vya watoto yatima na kutoa misaada.
Ambapo pia alisema kuwa pamoja na mafanikio hayo pia wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa wanachana ambapo wameomba kupitia ofisi ya Meya jiji la Arusha kuwasaidia katika mchakato wa upatikanaji wa mikopo inayotolewa na halmashauri kwani vijana wapo tayari kwaajili ya kuunda vikundi vya ujasiriamali.
Kwa upande wake Faraja Fredrick mmoja wa wakurugenzi katika shirika hilo hasa katika kituo namba 200 alisema kuwa dhumuni la umoja huo kuwaanda vijana kuja kuwa wafadhili kwani kwa muda mrefu maisha ya waafika hasa watanzania yamekuwa yakitegemea ufadhili kutoka nchi za nje lakini kupitia umoja huo wanaenda kutengeneza hamasa ya ufadhili wa ndani.
“Mzazi wao ni huu ufadhili tunataka tujenge kizazi ambacho kitafadhili na tuondoe dhana iliyojengeka tangu Karne ya Babu zetu kuwa ufadhili lazima utoke nje ambapo hadi sasa kwa takwimu nilizonazo umoja huu una vijana 220 lakini tunategemea wataendelea kujiunga hadi kufikia 1000 kwani vijana waliofadhiliwa na Compassion katika miaka 20 iliyopita ni zaidi ya 700.