MBUNGE wa Jimbo la Ukonga Jery Silaa ametoa ahadi ya fedha za Mfuko wa Jimbo shilingi milioni 5 zinatarajia kutolewa kwa ajili ya ukarabati wa shule ya sekondari Sangara Wilayani Ilala.
Mbunge Jerry aliyasema hayo Dar salaam Jana katika mahafali ya Sekondari ya Sangara iliyopo Mvuti kata ya Msongola .
“Nimezipokea changamoto za SHULE yenu ya Sangara ni shule kongwe ya mda mrefu ina itaji ukarabati ufanyike Ofisi yangu ya Jimbo la Ukonga nitachangia milioni 5 nitazielekeza kuwezesha ukarabati huo kutoka mfuko wa Jimbo .
Mbunge Jerry Silaa alisema pia atamshauri Afisa Elimu Sekondari Mwalimu Mussa afanye ziara katika shule hiyo kutatua kero mbalimbali.
Akizungumzia Jimbo hilo alisema Jimbo la Ukonga lina Shule za Sekondari 29 na shule za Msingi 60 amepongeza mahabara ya Sayansi shule ya Sangara ikiwemo mfumo wa Umeme zote kuongozwa na Wanafunzi wa kike ni ishara tosha Wanawake wanaweza.
Aliwataka Wanafunzi kuzingatia masomo ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao huku aliwataka wajiepushe na vishawishi mbalimbali ambavyo vinaweza kuwakatisha masomo.
Aliwatakia kheri Wanafunzi wote wa jimbo la Ukonga ambao wanaanza mitihani yao ya kidato cha NNE leo November 15/2021 akiwatakia wafanye vizuri ili wafaulu mitihani yao ili waweze kwenda chuo .
Alisema Taifa lolote ili kuweza kuendelea kiuchumi watu wake lazima wasome baadae wapatikane madaktari ,Walimu ,Watalam ,Mawaziri na Wabunge katika Jimbo la Ukonga amepokea fedha za Rais Samia Hassan Suluhu shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya madarasa 199 ya sekondari.
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari Sangara Frida Nyoni alisema jumla ya Wanafunzi 150 wamehitimu kati yao wasichana 118 na Wavulana 32 Walimu 22 kati yao Wanawake 15 wanaume saba jumla ya Wanafunzi shule nzima 813 wavulana 313 wasichana 500.
Mwalimu Nyoni alisema shule hiyo ya Sangara ilianzishwa rasmi 2007 inajivunia mafanikio mbalimbali kitaaluma ,sanaa, michezo na usafi wa shule
Mwisho.