Home LOCAL MASHIRIKA YASIYO YAKISERIKALI KENYA YAKABIDHI HATI YA KULIOMBA BUNGE LA EALA KUINGILIA...

MASHIRIKA YASIYO YAKISERIKALI KENYA YAKABIDHI HATI YA KULIOMBA BUNGE LA EALA KUINGILIA KATI SUALA LA USAWA WA KIJINSI KATIKA UONGOZI NCHINI KENYA

Mkurugenzi wa shirika la crown trust la nchini Kenya Daisy Amdany akikabidhi spika wa Bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki Martin Ngoga hati ya maombi ya kuitaka suluhisho la usawa wa kijinsia katika uongozi nchini Kenya.

Mkurugenzi wa shirika la crown trust Daisy Amdany wakiwaelezea wanahabari juu ya hati waliyoikabidhi kwa Spika wa Bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki.


Spika wa Bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki Martin Ngoga akiongea baada ya kukabidhiwa hati ya maombi ya kuingilia kati suala la uswa wa kijinsia katika uongozi nchini Kenya.

Baadhi ya wanachana wa mtandao wa masiliano na maendeleo ya wanawake bara la Afrika wakiwa katika picha ya baamoja baada ya kufungwa kwa kongamano lao lilifanyika mkoani Arusha.

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

Mashirika yasio ya kiserikali kutoka nchini Kenya   yakiongozwa na shirika la Crown Trust yamemkabithi hati ya maombi kwa  spika wa Bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Mh Martin Ngoga ya kuitaka Kenya kufuata matakwa ya katiba yao kutokana na kutokuwa na theluthi mbili ya wanawake katika uongozi nchini humo kama katiba ya nchi hiyo inavyoelekeza.

Akikabidhi hati hiyo katika kongamano la wanawake bara la Afrika  lililofanyika mkoani Arusha Daisy Amdany mkurugenzi wa Shirika la Crown Trust la nchini Kenya linalofanya kazi na wanawake katika kupigania haki zao pamoja na kuhusishwa kwa wanawake katika kila nyanja ikiwemo uongozi, uchumi na kijamii alisema kuwa Kenya ni nchi ambayo iko mbele kwa Mambo mengi katika jumuiya hiyo lakini imeshindwa  katika masuala ya kuhusisha wanawake Kikatiba.

“Kenya tulijipatia katiba mpya mwaka 2010 na katiba hiyo inahusisha wanawake kikmilifu katika siasa na kuna unaasema kuwa hapawezi kuwa na Dhaidi ya thelusi mbili ya jinsia moja katika uongozi wa kisiasa na uongozi wowote lakini Bunge letu la kitaifa na katika uongozi wamekataa kabisa kutekeleza sheria hiyo,” Alisema Bi Daisy.

Alieleza kuwa kama mashirika ambayo sio yakiserikali wameenda mahakamani mara nyingi na wamepewa oder na mahakama 2020 kuwa  Bunge hilo livunjwe kutokana na kutokuwa na thelusi mbili ya jinsia moja katika uongozi kwani katika nchi zote za jumuiya ni Kenya tuu ndio hawajatekeleza suala hilo.

“Hiyo oder ya mahakama haijatekelezwa na Sasa tuko njiani kuelekea katika uchaguzi mkuu wa tatu chini ya katiba mpya Agust 2022 na hakuna mtu yoyote anayeshughulika na suala hilo ndio mana tunaliomba Bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki kutusaidia kutafuta suluhisho ili Kenya iweze kufuata sheria iliyopo katika katiba yao na isiwache akina mama nyuma,” Alisema.

Alifafanua kuwa ikiwa Kenya ambaye tayari ni mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika Mashariki lakini haisishi wanawake ambao ni wengi zaidi wananchi katika nchi hiyo na ikiwa watatengwa Kenya haitilii maanani kuhusisha kwa wanawake katika nyanja za uongozi.

“Uongozi Ni kitu muhimu kwasababu viongizi ndio wanaotupangia maisha kwani wanapanga bajeti na maendeleo ambayo yatafanyika katika nchi na ikiwa sauti ya akina mama haipo katika hizo meza inamaanisha mambo yetu hakuna na ikiwa Rais wetu na viongizi wanaweza kukataa kukubali Sheria kuu ya nchi inamaanisha ya kwamba hatuko katika hali nzuri tupo kwenye mteremko wa hatari kwani hatuwezi kujua ni Sheria gani nyingine kesho watatupilia mbali,” Alisema.

Kwa upande wake Spika wa Bunge la jumuiya ya Afrika Mh Martin Ngoga  Alisema kuwa amepokea hati hiyo na ataiwasilisha katika vikao vya Bunge ili kuona ni kwa namna gani wataweza kutafuta suluhu ya jambo ili kuweza kuzifanya nchi wanachana kustawi zaidi na kutokuwa na migogoro.

Hata hivyo kongamano hilo  limeandalia na mtandao wa mawasiliano na maendeleo ya wanawake bara la Afrika (FEMNET) kwa kushirikiana na kituo cha usuluhishi (CRC) kwa ufadhili wa shirika la IDEA

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here