Home SPORTS MASHABIKI 35,000 RUKSA KUCHEKI SIMBA Vs RED ARROWS

MASHABIKI 35,000 RUKSA KUCHEKI SIMBA Vs RED ARROWS

Na: Mwandishi wetu

MASHABIKI 35,000 ni ruksa kuushuhudia mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Novemba 28.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika,

(CAF) ni mashabiki hao wataruhusiwa kuwa ndani ya uwanja kushuhudia mchezo huo.

Na pia mashabiki hao wanapaswa kufuata taratibu na kanuni za kujilinda dhidi ya Corona.

Unatarajiwa kuwa mchezo mkali na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi.

Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco itakuwa ni kibarua chake cha kwanza katika mechi za kimataifa baada ya kurithi mikoba ya Didier Gomes.

Mchezo wa kwanza kukaa benchi ilikuwa dhidi ya Ruvu Shooting na alishinda mabao 3-1 ila ulikuwa ni wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Previous articleMAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 26-2021
Next articleSIMBA WATAJA KIINGILIO CHA RED ARROWS
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here