Na: Stella Kessy
KIKOSI cha KMC FC leo kimefanya maandalizi yake ya mwisho kuelekea katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara hapo kesho dhidi ya Mbeya City utakaopigwa katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya saa 16:00 jioni.
Mchezo huo wa mzunguko wa saba, KMC FC itakuwa ugenini, na kwamba hadi sasa benchi la ufundi kwa kushirikiana na wachezaji pamoja na viongozi limefanya maandalizi ya kutosha na kwamba kikosi kipo tayari katika mtangane huo.
Akizungumza baada ya mazoezi kocha Mkuu John Simkoko amesema kiwa wamejipanga vema kuhakikisha wanafanya vyema mchezo licha ya kuwa mchezo utakuwa na ushindani mkubwa lakini kama Timu kikubwa nikupambania alama tatu muhimu ambapo kimsingi mchezo huo bado upo ndani ya uwezowetu.
“Tunaifahamu Mbeya City kuwa ni timu nzuri, na tunacheza ugenini, lakini bado tupoimara na tunaingia uwanjani kutafuta alama tatu muhimu ambazo kimsingi kila mmoja anazihitaji na sisi KMC FC tumekuja hapa Mbeya kuzitafuta hizo pointi hivyo maandalizi ambayo tumeyafanya tangutulipokuwa Dar es Salaam hadi sasa yatakwenda kutupa matokeo chanya.
Kikosi hicho cha KMC kilifika Jijini jana salama, licha ya kwamba hali ya hewa ni baridi iliyotawaliwa na mvua na leo wachezaji wapo salama wamefanya mazoezi katika uwanja ambao watautumia kesho kwenye mchezo wao hivyo kikubwa tunamuomba mwenyezi Mungu atuamshe salama ili tukapambane uwanjani vizuri.