Home SPORTS KMC, AZAM VITANI LEO

KMC, AZAM VITANI LEO

Na: Stella Kessy

KLABU ya KMC FC  leo wanashuka dimbani kuchuana na Azam FC katika mchezo wa  Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara mchezo utakaochezwa katika  dimba la Uhuru Jijini Dar es  Salaam utakaochezwa majira ya saa 16:00 kamili jioni.

Mchezo huo wa mzunguko wa sita tangu kuanza kwa ligi kuu ya NBC , huku Kikosi cha KMC leo wanakuwa wenyeji wa mchezo huo.

Mpaka sasa KMC wanajumla ya michezo mitano na wana pointi 2 na wapo katika nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi,huku Azam wapo nafasi ya tisa na wanajumla ya pointi 7 katika msimamo wa ligi.

Kikosi cha KMC  kipo chini ya Kocha mkuu John  Simkoko na  msaidizi wa wake , Habibu Kondo amesema kuwa licha ya kuwa Timu haina  matokeo mazuri lakini maandalizi yaliyofanyika katika kipindi hiki cha mapumziko yaliyokuwa yamepisha Timu ya Taifa yamefanikiwa kwa asilimia kubwa ikiwemo kurekebisha changamoto mbalimbali ambazo zilionekana katika michezo hiyo.

Habibu amefafanua kuwa hali ya kikosi ni nzuri  ,ikiwemo morali za wachezaji ipo juu pamoja na fitness nzuri na kwamba licha kuwa mchezo wa kesho utakuwa na ushindani mkubwa lakini kwa maandalizi ambayo yamefanyika yataleta matokeo mazuri.

Kondo ameongeza kuwa mipango ya Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni nikufanya vizuri katika michezo ya Ligi kuu ya NBC  na kwamba licha ya kuwa na mwanzo ambao siorafiki lakini bado matumani makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho nimkubwa.

“Tunajua kuwa hatujaanza vizuri kwenye michezo yetu, lakini bado tupo kwenye ubora wetu, tumefanya maandalizi ambayo kimsingi yataleta matokeo chanya kikubwa mashabiki zetu wazidi kutupa ushirikiano.

Aidha Kondo ameongeza kuwa” Tunaenda kucheza na Azam ambayo ni Timu nzuri na tunawaheshimu lakini tutapambana kuhakikisha kwamba tunaondoka na alama tatu kwani mchezo upo ndani ya uwezo wetu.

Kwa upande wa kikosi cha Azam Kocha msaidizi Vivier  Bahati amesema kuwa kikosi chake kina maandalizi ya kutosha na  wachezji wapo vizuri kwa ajili ya kufanya vyema.

Katika mchezo wa leo wachezaji wamepanga kufanya mapinduzi japo KMC ni timu nzuri na inawachezaji vijana na mechi ya leo itakuwa ngumu dhidi yao.

“Kweli Azam inakikosi kizuri na tutahakikisha kufanya vizuri leo kwani tunatambua kuwa wapinzani wetu wamejipanga na wanakikosi kizuri lakini hatuwezi kuwahofia kwani kikubwa ni dakika 90 za kupambana” amesema.

Aliongeza kuwa katika kikosi hicho kitaendelea kuwakosa wachezaji ambao walipewa adhabu na klabu pia prince dube  ambaye ameanza mazoezi kidogo.


 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here