WADAU wa sekta ya usafirishaji kwa njia ya meli wamekutana jijini Dar es Salaam kushuhudia uzinduzi wa kitabu cha Enhancing your Knowledge in Shipping ambacho kimeeleza hatua kwa hatua mchakato wa kuagiza na kusafirisha mizigo kwa usafiri wa meli.
Kitabu hicho ambacho ni cha kwanza kabisa kuandikwa katika tasnia ya usafirishaji mizigo kwa meli nchini kimeandikwa na Mtanzania mbobezi katika tasnia ya usafirishaji mizigo kwa meli Julius Nguhula ambaye ameandika kitabu hicho kwa ajili ya kuhakikisha watanzania na wadau wa sekta ya bahari wanakuwa na elimu ya kutosha katika eneo hilo
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro Dk.Charles Kimei ambaye ametumia nafasi hiyo kuzungumzia umuhimu wa wadau wa sekta ya bahari hasa eneo la usafirishaji mizigo kwa meli kuhakikisha wanakuwa na kitabu hicho ambacho kimejaa kila aina ya maarifa na kwamba kimekuja wakati muafaka ambapo Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi wameamua kusimama kidete katika kuhamasisha uchumi wa buluu unaotokana na uwepo wa bahari,hivyo kitabu kimekuja kwa wakati muafaka.
Mh.David Kihenzile mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini na mwenyekiti wa Bunge akizungumzia kitabu hicho namana kitakavyosaidia wabunge kujadilia masuala ya ueneshaji wa Bandari na Meli kwa weledi kuoitia kitabu hicho.
Mtanzania mbobezi katika tasnia ya usafirishaji mizigo kwa meli Julius Nguhula aliyetunga kitabu cha (Enhancing your Knowledge in Shipping) ambacho kimeeleza hatua kwa hatua mchakato wa kuagiza na kusafirisha mizigo kwa usafiri wa meli. akiwa na Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro Dk.Charles Kimei wa pili kutoka kushoto, Mh.David Kihenzile mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini na mwenyekiti wa Bunge kushoto pamoja na Emmanuel Malya Mwenyekiti wa Kampuni ya Maritine Group na John Massawe Mwenyekiti wa Chama Tanzania Shipping Agents Asocciation T(ASAA) kulia wakionesha kitabu hicho mara baada ya kuzinduliwa rasmi leo kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es Salaam.
Mtanzania mbobezi katika tasnia ya usafirishaji mizigo kwa meli Julius Nguhula akipiga picha na baadhi ya wanafunzi wake mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho kuzinduliwa.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla hiyo.
Baadhi ya wanakamati wa kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo wakiwa katika picha ya pamoja.