Home SPORTS HITIMANA AFURAHISHWA NA KIWANGO CHA WACHEZAJI WAKE

HITIMANA AFURAHISHWA NA KIWANGO CHA WACHEZAJI WAKE

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Na: Stella kessy, DAR ES SALAAM.

KAIMU Kocha Mkuu Hitimana Thiery  amesema kuwa amefurahishwa na kiwango walichoonyesha kiungo  mshambuliaji Ibrahim Ajibu.

Ajibu aliingia kipindi cha pili na kuongeza ufundi katika idara ya ushambuliaji kwa kupiga pasi na kuwafungua  Namungo ambao muda mwingi walikuwa wanazuia.

Hitimana amesema Ajibu ni mchezaji mzuri ingawa hajapata nafasi kubwa ya kucheza lakini kuwa bado wana mechi nyingi na mashindano mbalimbali atazidi kuonekana uwanjani.

Ajibu ni mchezaji mzuri ana kipaji kikubwa tulimuingiza baada ya kuona Namungo wanacheza sana faulo na ajibu ni mzuri kwenye mipira ya adhabu tulijua atatusaidia na kweli  ametimiza malengo yetu” amesema.

Katika mchezo wa jana ajibu ndio aliyeanzisha mpira wa adhabu kwa Mohamed Husen ambaye alipiga krosi iliyounganishwa kwa kichwa na Medie Kagere na kutufungia bao la ushindi.