Home SPORTS GSM YADHAMINI LIGI KUU SOKA BARA KWA BILIONI 2.1

GSM YADHAMINI LIGI KUU SOKA BARA KWA BILIONI 2.1


 Na: stella Kessy, DAR ES SALAAM.

KAMPUNI ya GSM Group of companies leo imeingia mkataba wa udhamini mwenza wa kuidhamini ligi kuu soka Tanzania bara kwa thamani ya shilingi Bilioni 2.1 kwa muda wa miaka 2.

Akizungumza na wanahabari leo Eng. Hersi Said kutoka kwenye kampuni ya GSM amesema wameingia mkataba huo lengo likiwa ni kuongeza nguvu katika vilabu vya soka hapa nchini.

“Hatuwezi kuwa na timu ya taifa bora kama hatuna vilabu ambavyo haviko imara kifedha na hili tumeliona na ndio maana tumeona ni vyema kuongeza nguvu katika jitihada  za kusaidia soka hapa nchini” amesema Eng. Hersi

Ameongeza kuwa udhamini huu hauna uhusiano wowote na vilabu vyovyote wanavyovidhamini vikiwemo Yanga SC, Coastal Union, Namungo FC na vilabu vingine wala mahusiano ya upangaji wa wowote wa matokeo.

Naye makamu wa pili wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Athumani Nyamlani amesema fedha hizo za udhamini zitatumika kwa manufaa ya klabu na timu zinazoshiriki ligi kuu.

“Ligi ya Tanzania imekuwa bora ikiwemo Ligi Kuu imekuwa na ubora zaidi katika bara la Afrika na huu ubora tunatarajia wadhamini wengine kujitokeza

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here