Ni Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Pulina Gekul akiongea katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukizwa yanayoadhimishwa kitaifa mkoani Arusha. |
Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Paulina Gekul akizindua muongozo wa mazoezi uliondaliwa na wizara ya Afya wanaoshirikiana nae ni viongozi mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela na wengine ni kutoka sekta mbalimbali za afya .
kaimu Mkurugenzi wa huduma za tiba kutoka wizara ya Afya Dkt Vivian Timothy Onanji akielezea muongozo iliyotolewa mahususi kwaajili ya mazoezi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akiongea katika maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukizwa yanayoendelea mkoani Arusha.
Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Pulina Gekul, mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela, Kaimu Mkurugenzi wa huduma za tiba kutoka wizara ya Afya Dkt Vivian Timothy Onanji na kaimu katibu tawala wa mkoa wa Arusha Agney Chitukuro wakionuesha muongozo wa mazoezi uliozinduliwa katika maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukizwa.
Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Arusha kutoka tasnia na mashirika mbalimbali wakifanya mazoezi katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukizwa yanayoendelea katika viwanja vya Sheikh Amri abeid.
Naibu waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Pulina Gekul na mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela wakioshiriki katika kufanya mazoezi ikiwa nisehemu ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukizwa.
NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Naibu waziri wa utamaduni Sanaa na michezo Pulina Gekul amewataka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kote nchini kuunda vikundi vya mazoezi (Jogging clubs) katika maeneo yao ili kuweza kupambana na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kutokana na ongezeko kubwa la magonjwa hayo yanayosababishwa na aina za maisha.
Gekul aliyasema hayo wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza ambapo alisema kuwa mfumo wa maisha uliopo kwa sasa ni hatari kwa afya hasa kwa watumishi wa umma kutokana na kutekeleza majukumu yao wakiwa wamekaa ambapo wakifanya mazoezi kwa makundi makundi mbalimbali itasaidia kupunguza ukubwa wa tatizo hilo.
Alisema kuwa katika jamii zetu magonjwa hayo yamekukwa yakianza mapema na kuzorotesha nguvu kazi ya taifa kwani vijana pia ni waadhirika wa magonjwa hayo kutokana na aina ya maisha wanaoishi ikiwemo ulaji, matumizi ya pombe, sigara na madawa ya kulenywa
“Nitoe rai kwa wananchi wote na watumishi kushiriki kushiriki katika mazoezi kabla ya kazi na baada ya kazi kwani awali magonjwa haya yalikuwa kwa asilimia 20 na sasa asilimia 33 na tunategemea yatafikia asilimia 40 kama hatua madhubuti hazitachukuliwa juu ya kubadili aina za maisha kwa kufanya mazoezi lakini pia kuzingatia lishe sahihi,”Alisema Gekul.
Alifafanua kuwa magonjwa haya sio tishio tu kwa nchi ya Tanzania bali ni kwa ulimwengu wote ambapo kwa takwimu za mwaka 2016 yanasababishwa vifo milioni 41 sawa na asilimia 71 Duniani kote.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa huduma za tiba kutoka wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Vivian Timothy Onanji alisema kuwa kinachohitajika ili kuleta faida za kiafaya na kupunguza athari zitokanazo na tabia ya kutokujishugulisha kwa mara ya kwanza yametolewa mapendekezo yanayohusisha tabiabwete miongoni mwa makundi maalum kama vile wajawazito, waliojifungua,wanaoishi na maradhi sugu na wenye ulemavu ambopo lengo la mpango huo wa kidunia ni kupunguza tabia ya kutokujishugulisha kwa asilimia 15 ifikapo mwaka 2030.
Alisema kuwa muongozo huo umetoa mapendekezo muhimu ya kiafya kwa watu wa rika tofauti kwanzia miaka 5 hadi 64 na zaidi bila kujali tofauti za kijinsia, tamaduni, hali ya kiuchumi na kuendelea ambapo magonjwa yasiyoambukiza yanajumuisha magonjwa ambayo hayawezi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kama vile shinikizo la juu la damu, Saratani, Kisukari, Pumu, magonjwa ya akili, Siko seli, Ajali na baadhi ya magonjwa ya macho, kinywa, masikio, pia na koo.
Aidha Alisema kuwa muongozo wa mazoezi umeandaliwa kufuatia uchambuzi yakinifu wa sera, sheria, kanuni na miongozo ya ushughulishaji mwili hapa nchini ambapo ulihusisha taasisi na sekta zote kutoka pande zote za Jamuhuri ya muunganao wa Tanzania.
Naye mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela Alisema kuwa kama mkoa wataendelea kuinzi na kuheshimu fursa hiyo waliyopewa na kwa wiki nzima ya maadhimisho hayo watashiriki kikmilifu ili kuweza kufikia lengo la kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza.