Home LOCAL DKT GWAJIMA KUONGOZA MAWAZIRI WENZAKE WATATU KUHUDHURIA MAADHIMISHO WIKI YA MAGONJWA...

DKT GWAJIMA KUONGOZA MAWAZIRI WENZAKE WATATU KUHUDHURIA MAADHIMISHO WIKI YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA ARUSHA.

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Waziri wa sanaa na michezo,Innocent Bashungwa anatarajiwa kuzindua  maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukizwa yanayofanyika kitaifa  mkoani Arusha mnamo Novemba 6 mwaka huu kwa kuanza na ajenda ya  mazoezi mazoezi na umakini kwenye lishe.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho hayo ambapo alisema kuwa kwa  kauli mbiu kwa mwaka huu ni isemayo “badili mtindo wa maisha borsha afya”  mazoezi na umakini katika lishe yatazingatiwa.

“Vyakula tunavyokula tunapaswa kuepuka sukari nyingi, mafuta, na chumvi lakini vilevile kuzingatia katika kufanya mazoezi kwani vitu hivi ni muhimu kuzingatia katika kupambana na magonjwa yasiyo ambukiza,” Alisema Mongela.

Alifafanua kuwa kumekuwa na juhudi kubwa za kuzuia na kupambana na magonjwa yasiyoambukiza ambayo pia muheshimiwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania  Samia Hassan Suluhu amekua akishiriki kupambana nayo kwanzia akiwa makamu wa Rais na hata sasa ambapo katika maadhimisho hayo kutakuwa na huduma za upimaji na utoaji ushauri wa utakaofanya na wataalamu.

Aidha alieleza kuwa katika kuadhimishwa wiki ya magonjwa yasiyoambukizwa kuanzia November 11 na 12 wanaotarajia Mhe Joyce Ndalichako waziri wa Elimu sayansi na teknolojia pamoja na Mhe Ummy Mwalimu waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa wataweza kuhudhuria katika maadhimisho hayo.

Aliendela kusema kuwa kilele Cha maadhimisho hayo itakuwa ni November 13 ambapo wanatarajia mgeni rasmi kuwa waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Dorothy Ngwajima ambapo ambaye ndiye atakayehitimisha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here