Home SPORTS DKT. ABBAS AWAHAMASISHA WATANZANIA KUJITOKEZA KUSHUHUDIA MICHUANO YA Canaf

DKT. ABBAS AWAHAMASISHA WATANZANIA KUJITOKEZA KUSHUHUDIA MICHUANO YA Canaf

 

Mwandishi wetu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Hassan Abbas amewataka Watanzania kujitokeza katika Mashindano ya Bara la Afrika kwa Mchezo wa Mpira wa Miguu wa Watu wenye Ulemavu (CANAF) na kuzishangilia timu zote ili kuonesha ukarimu wa watanzania.

Hayo ameyasema jana  wakati wa kikao na Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo kufanya tathmini ya mafanikio na changamoto katika kila kamati ili kuboresha na kuyafanya yafanyike kwa ufanisi mkubwa.

“Ukarimu wetu ni muhimu, watanzania tujitokeze kushangilia timu zote katika mashindano haya, siyo wakati wa timu yetu ikicheza tu,”alisisitiza Dkt. Abbasi na kuongeza kuwa:

“Watanzania tuendelee kuupiga mwingi Tanzania tuna vipaji na vipawa, na kila mtu awe balozi wa mashindano haya,”alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here