Home LOCAL DIWANI TUMIKE MALILO AMPONGEZA RAIS SAMIA SULUHU

DIWANI TUMIKE MALILO AMPONGEZA RAIS SAMIA SULUHU



NA: HERI SHAABAN

DIWANI wa Kata ya Bonyokwa Wilayani Ilala ,Tumike Malilo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu kwa utekelezaji wa Ilani kwa vitendo .

Diwani Tumike alisema hayo Dar es Salaam jana wakati wa kukabidhi vifaa vya Mahara kwa ajili ya shule ya Sekondari Bonyokwa  wilayani Ilala ,vifaa alivyopewa na Serikali kwa ajili ya shule hiyo.

“Natoa pongeza kwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassani Suluhu  katika sekta ya Elimu Kata yangu imepata mgao wa fedha kwa ajili ya madarasa ujenzi unaendelea na leo nimepewa vifaa vya  mahabara ili Wanafunzi wasome kwa vitendo” alisema Tumike .

Tumike alisema shule ya Sekondari ya Bonyokwa ya Serikali ina Wanafunzi wa Kidato cha kwanza mpaka kidato cha pili shule mpya .

Aidha Tumike aliwataka wazazi kujenga tabia ya Wazazi kukagua daftari za Wanafunzi wao kila wakati ikiwemo kushirikiana na Walimu wao ili kukuza taaluma.

Aliwataka Wanafunzi wa shule ya sekondari Bonyokwa pamoja na walimu wa shule hiyo kuvitunza vifaa hivyo vya mahabara ili watumie katika masomo yao.

Wakati huohuo Tumike aliwapongeza Walimu na Wanafunzi wa shule ya Msingi Bonyokwa kwa ufaulu mzuri katika shule yao jumla ya Wanafunzi 164 wamefaulu kwenda kidato cha kwanza kati ya Wanafunzi 172 ambapo Wanafunzi wanane wameferi.

“Natoa pongezi Idara ya Elimu Msingi Halmashauri ya Jiji Afisa Elimu Elimu Mwalimu Sipora Ntenga kwa  kusimamia vizuri sekta ya Elimu Msingi kupelekea Wilaya ya Ilala kushika nafasi ya kwanza Kitaifa” alisema

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Bonyokwa Mwalimu Pendo William alisema shule hiyo ina Wanafunzi wa kidato cha Kwanza mpaka kidato cha pili.

Mwalimu Pendo William alisema kidato cha pili wapo 262 Wasichana 125 wavulana 137,kidato cha kwanza  332 wavulana 179 wavulana na wasichana 153  na Walimu 14 Walimu wanawake 12 na Walimu wa kiume wawili.

Mwisho

Previous articleMAGAZETI YA LEO J.TANO NOVEMBA 10-2021
Next articleBODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO (CPB) KUUZA NAFAKA NCHINI KENYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here