Home LOCAL DCEA YAELEZA JINSI WANAWAKE WANAOTUMIA DAWA ZA KULEVYA WANAVYOAMBUKIZWA UKIMWI

DCEA YAELEZA JINSI WANAWAKE WANAOTUMIA DAWA ZA KULEVYA WANAVYOAMBUKIZWA UKIMWI

Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya nchini (DCEA) Dkt. Peter Mfisi akizungumza kwenye Kikao Kazi cha waandishi wa habari za Kidigitali kilichoandaliwa na Mamlaka hiyo Mjini Morogoro.


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka (DCEA) Florence Khambi akitoa mada ya ufunguzi kwenye kikao kazi hicho kilicho.

Mtaalamu wa masuala ya Mitandao Dotto Mnyadi akitoa mada kwenye Kikao Kazi hicho kwa waandishi wa habari.

 

Na: Hughes Dugilo, MOROGORO

Imeelezwa kuwa asilimia kubwa ya wanawake wanaotumia Dawa za Kulevya hawafiki kwenye vituo vya matibabu kutoakana na kuhofia kunyayapaliwa.

Utafiti umeonesha kuwa kati ya wanawake 100 wanaotumia Dawa za kulenya nchini 61 kati yao wameambukizwa virusi vya ukimwi kutokana na kuchangia sindano za kujidunga.

Hayo yameelezwa na Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) Dkt. Peter Mfisi alipokuwa akizungumza kwenye kikao kazi cha waandishi wa habari za Kidigitali kilichoandaliwa na Mamlaka hiyo Mkoani Morogoro, nakwamba utafiti huo ulifanyika mwaka 2014 ambapo mpaka sasa bado haujafanyika utafiti mwingine.

Kamishna Mfisi ameeleza kuwa kutokana na tatizo hilo, Mamlaka imejipanga kuanzisha Kliniki maalumu za waraibu wa Dawa za kulevya zitakazowasaidia waraibu wa kike kupata matibabu kwa wakati nakwamba Kliniki hiyo itawaondolea tatizo la kuwa na hofu ya kunyanyapaliwa.

Amesema kuwa lengo kuu la Kikao kazi hicho ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuihabarisha jamii ya Kitanzania hususani waathirika wa Dawa za kulevya pamoja na Virusi vya Ukimwi ili kuchukua hatua stahiki za kimatibabu.

“Lengo kuu la Kikao Kazi hiki ni kutaka kuifikia jamii kupitia ninyi wanahabari kuihabarisha jamii ifahamu juhudi za Mamlaka katika mapambano ya Dawa za Kulevya na nini wanapaswa kufanya hasa wanapoona kuna waathirika miongoni mwao” Amesema Kamishna.

Aidha ameongeza Kliniki hizo zitakuwa na uwezo wa kuwahudumia watoto wadogo waliozaliwa na uraibu ambao kwa kiasi kikubwa huwa wanazaliwa wakiwa na tatizo la arosto kutokana na matumizi ya Dawa za kulevya kwa mama mjamzito.

“Watotot wengi wanaozaliwa na wakinamama wanaotumia Dawa za Kulevya wanakuwa na arosto, (Neonatal abstinence Syndrome), hivyo Klinik hizo zitakuwa na uwezo wa kuwasaidia watoto wote waliozaliwa na tatizo hili” Ameongeza.

Kikao Kazi hicho cha siku tatu kinachoendelea Mjini Morogoro kimewakutanisha waandishi wa habari za kidigitali kutoka vyombo 30 vya habari mtandao kilianza rasmi tarehe 10 na kinatarajiwa kuhitimishwa tarehe 12 Novemba Mwaka huu

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here