Home LOCAL DC LUDIGIJA AMPONGEZA MHE RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUIPATIA ILALA FEDHA...

DC LUDIGIJA AMPONGEZA MHE RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUIPATIA ILALA FEDHA SEKTA ELIMU

 

Na: Heri Shaaban (Ilala)

MKUU  wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzamia Samia Hassan Suluhu, kuwapatia shilingi Bilioni 5.1 fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa idara ya Elimu Sekondari madarasa 255

Mkuu wa Wilaya Ludigija alitoa pongezi  hizo katika ziara yake na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Ilala, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji, Meya wa Halmashauri hiyo na Wataalam, katika kufatilia ujenzi huo .

“Nampongeza Rais wetu kuwekeza katika sekta ya Elimu ametupatia fedha za kutosha shilingi Bilioni 5.1 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya UVIKO -19  ujenzi unaendelea vizuri tutasimamia fedha hizi kufanikisha ujenzi wa madarasa 255 “alisema Ludigija


Alisema ziara hiyo ni endelevu kukagua madarasa ya shule za zote za Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam lenye shule 41 jana amefanikiwa kukagua shule kumi  kati 41  ambazo zinajengwa madarasa ya UVIKO 19.

Mkuu wa Wilaya Ludigija ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa kwa baadhi ya shule alizozitembelea  huku akisema ziara hiyo ni endelevu  akitoa pongezi kwa wasimamizi wa ujenzi wa shule hizo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Jumanne Shauri, Meya wa Halmshauri ya Jiji Mhe. Omary Kumbilamoto na Watendaji wake wa Idara ya Elimu Sekondari pamoja na kamati za Ujenzi za Shule na Walimu wote .

“Nichukue nafasi hii kuwapongeza walimu, kamati zote za shule za ujenzi kwa kazi kubwa ambayo nimeiona imefanyika kwa maeneo ambayo nimetembelea, lakini wito wetu sisi kama Wilaya na kama ambavyo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesema fedha hizi zisimamiwe vizuri  na kuleta tija tunamuahidi kutekeleza maelekezo yake kwa weledi na tunataka tuone ujenzi huu unakamilika kwa wakati lakini kwa kuzingatia ubora” amsema


Aidha, Shule zilizotembelewa siku ya leo ni pamoja na Shule ya Sekondari Dar es Salaam yenye vyumba vya madarasa (05) Gerezani (04) Kinyerezi (08) Kinyerezi Mpya (03) Magole (12) Kipunguni (08) Misitu (04) Kerezange (08) Kitunda (12) na Minazi Mirefu (08)

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,  Jumanne Shauri ametoa hofa  katika kuwaongezea kasi ya usimamizi wakuu wa shule zenye miradi hiyo, ametoa motisha ya Shilingi Laki Tano (500,0000/=) kwa atakayefanya vizuri zaidi, Shilingi Laki Tatu (300,000/=) kwa atakayefuatia na Shilingi Laki Mbili (200,000/=) kwa atakayekuwa nafasi ya tatu (3).

Mkurugenzi Shauri aliwataka Walimu wa shule hizo kushirikiana katika kufanikisha ujenzi huo unaisha kwa wakati na mda uliopangwa na Serikali Desemba 15/2021 madarasa yawe yamemalizika .

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here