Home LOCAL DC JOKATE AKAGUA MIUNDOMBINU YA MASOKO WILAYANI TEMEKE

DC JOKATE AKAGUA MIUNDOMBINU YA MASOKO WILAYANI TEMEKE




DAR ES SALAAM.

MKUU wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo amefanya ziara ya ukaguzi wa miundombinu katika maeneo ya masoko waliyohamishiwa wafanyabiashara Wadogo maarufu Machinga, leo Novemba 10,2021 huku akiambatana na baadhi ya viongozi na wakuu wa idara za halmashauri ya manispaa ya Temeke.

Katika ziara hiyo mkuu wa Wilaya amesisitiza kukamilishwa kwa miundombinu ya maji na matundu ya vyoo kwenye maeneo hayo ya kufanyia biashara ili kuweka mazingira rafiki kwa Wafanyabiashara, na kuendelea kuvutia wengine waliopo maeneo yasiyo rasmi.

Hata hivyo Jokate amewataka Watendaji na maafisa biashara wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanashirikiana na Serikali kuhamasisha wafanyabishara hao kutoka barabarani na kwenda  kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wao kufanya biashara.

“Haiwezekani Serikali inaweka mikakati mizuri ya kuwasaidia Wananchi,lakini watu wachache wanataka kukwamisha hili zoezi, kiukweli hatutawavumilia na tutawashughulikia” alisema Jokate.

Kwa upande waka Ofisa Biashara wa  Manispaa ya Temeke Ramadhani  Gurumukwa ametoa siku 14 kuanzia leo, kwa wafanyabiashara waliopewa vizimba katika maeneo rasmi kuhamia , na  ikiwa watashindwa, baada ya siku hizo vizimba vyao watapewa Wafanyabiashara wengine ambao wako tayari kutii maelekezo.

Masoko yaliyotembelewa na Mkuu huyo Buza Sigara, Kanisani -Savoi, Mbagala Saku, Kiramba, Charambe na Mbande huku akikiri kuridhishwa na kazi inayofanywa na viongozi wa Wamachinga katika kuhimiza ufanyaji wa biashara kwenye maeneo yanayotambulika na Serikali,na kumuagiza kamanda wa polisi Temeke kuhakikisha vyombo vya usafiri wa Abiria vinafika katika vituo vilivyo jirani na  masoko hayo,na sio kugeuzia njiani.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here