Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Muleba Ndugu Athumani Kahara akiyoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Kabitembe katika kata ya Kabitembe kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba Ndugu Toba Nguvila ikiwa sehemu ya ziara yake pamoja wa Wajumbe wa Sekretarieti wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mkoani Kagera ya kukagua, kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Muleba Ndugu Toba Nguvila (kulia) kukagua ujenzi wa madarasa ya shule ya Kabitembe ikiwa sehemu ya ziara yake pamoja wa Wajumbe wa Sekretarieti wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mkoani Kagera ya kukagua, kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akishiriki ujenzi wa madarasa ya shule ya Kabitembe pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge ikiwa sehemu ya ziara yake pamoja wa Wajumbe wa Sekretarieti wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mkoani Kagera ya kukagua, kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025. ( Picha na CCM Makao Makuu)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo amewataka Viongozi wa Chama cha Mapinduzi kujiheshimu kwa kutekeleza kila wanachoahidi.
Katibu Mkuu amesema hayo wakati akihitubia wakazi wa shina namba 5 Kitumu, Tawibla Rulanda kwa Balozi James Bahindi.
“Kazi ya siasa si uongo, kazi ya siasa si majungu, kazi ya siasa sio fitna, kazi ya siasa sio umbea, kazi ya siasa sio kusingiziana, kazi ya siasa ni kuombeana mema, kazi ya siasa ni kupendana, kazi ya siasa ni kushikamana, kazi ya siasa ni kuwaniana mema mwenzio” alisema Katibu Mkuu.
Katika ziara yake Wilayani Muleba mkoa wa Kagera , Katibu Mkuu wa CCM amekagua na kuhamasisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 .