Home SPORTS CHEKA NA ALI KASUSU KUZICHAPA DISEMBA 3

CHEKA NA ALI KASUSU KUZICHAPA DISEMBA 3

Na: Stella kessy

KAMPUNI  ya  Grobox sports promotio wameandaa pambano  kati ya Cosmas Cheka na Muhsini Swalehe ‘Alkasusu’  litakalofanyika Disemba 3 mwaka huu katika kiwanja cha Kinesi Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari  promota wa ngumi Siah Duncan amesema kuwa pambano hilo lina jumla ya mapambano mengine matano ya utangulizi huku moja likiwa na wanawake. 

Katika pambano hilo ambalo litakuwa na jina la usiku wa Mishindo ambapo kila bondia atakuja na mshindo wake 

Kwakweli hili pambano litakuwa na mshindo kwa mabondia ambao watashiriki kwani ninatambua kila bondia ambaye anapambana katika pambano hilo likatako kuwa  mshindo wa aina yake” alisema.

Kwa upande wa Skawa Junior meneja wa vipindi wa TV3  amesema kuwa lengo la kuonyesha pambano hilo ni kuwafikia watu wa chini pamoja na wakati sababu Startimes ni kung’amuzi  ambacho hakina gharama kubwa na ni rafiki kwa watanzania.

“Hii ni tv ambayo Haina muda mrefu lakini ni tv inayoonyesha michezo muda mrefu pamoja na burudani na imefanya mapinduzi makubwa katika suala la michezo ya aina yote”

Amesema kuwa wameamua kuungana na probox sababu wamekuwa kufanya hivyo ili kuwafikia watu wa hali ya chini na hali ya Kati watu wengi ambao wapo katika maisha na wanakosa burudani kwa sababu ya gharama lakini pia unaweza kuangalia vipindi kupitia simu yako inakupa nafasi kama upo mbali na televishen.

Katika usiku huu wa mshindo tumejipanga kuhakikisha wanatoa burudani pamoja na ubora wa tv yao.

Pambano Hilo ambalo litaanza kuanzia saa 12 jioni mpaka litakapo malizika.

Kwa upande wa bondia Cosmas Cheka alisema kuwa amejipanga kuhakikisha anafanya vyema katika  pambano hilo.

Pia kwa mpinzani wake  Muhsini Swalehe ‘Alkasusu’ amemtaka bondia  Cosmas kuacha maigizo aje siku ya pambano kwani amejipanga vyema kuhakikisha anaibuka na ushindi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here