Home SPORTS BWALYA: TUNAPAMBANA KUSONGA MBELE SHIRIKISHO

BWALYA: TUNAPAMBANA KUSONGA MBELE SHIRIKISHO

 

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

Kiungo mshambuliaji wa Simba Rally Bwalya amesema baada ya kukosa nafasi ya kuingia katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa sasa ni wakati wa kufanya hivyo katika michuano ya Kombe la shirikisho Afrika.

Kiungo huo mzambia ameweka wazi kuwa malengo ya wachezaji pamoja na benchi la ufundi ni kuhakikisha wanaingia makundi kwa kuitoa Red Arrows.

Bwalya amesema mchezo wao wa kwanza  dhidi ya  Arrows hao utakuwa mgumu kwa sababu wapinzani nao wanataka kutafuta matokeo ugenini ili kurahisisha mechi ya marudiano lakini kikosi cha simba kimeshawakabiri kwa michezo yote miwili.

“Red Arrows  si timu mbaya ndio maana imefika hatua hii na hautaidharau tutaingia uwanjani kupambana kutafuta ushindi tukijua upo nyumbani, tunaingia uwanjani kuhakikisha tunapambana kutafuta ushindi” amesema.

ameongeza kuwa walipokuwa katika nafasi ya kuingia hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa lakini ikashindikana, sasa tumepata tena nafasi ya kufanya hivyo  kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika watahakikisha wanafanya vyema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here