Home SPORTS BOCCO AWAPIKU MANURA, ZIMBWE JR, TUZO ZA IDFA

BOCCO AWAPIKU MANURA, ZIMBWE JR, TUZO ZA IDFA

Na: Stella Kessy

NAHODHA John Bocco  ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2020 wa mashabiki zilizotolewa na chama cha Soka Wilaya ya Ilala (IDFA).

Bocco amemshinda mlinda mlango Aishi Manura na mlinzi wa kushoto Mohamed Hussen Zimbwe jr katika halfa ya tuzo hizo zilizofanyika ukumbi wa Hotel ya Lamada jijini Dar es Salaam.

Katika msimu wa mwaka 2020/2021 ulikuwa bora kwa nahodha  Bocco kutokana na kushinda tuzo nyingi binafsi kama mfungaji bora wa ligi na mchezaji bora wa mwaka (MVP).

Katika halfa hiyo pia klabu ya simba imeshinda tuzo ya klabu bora ya mwaka kutokana na mafanikio makubwa  waliyopatikana.

Kwa msimu wa 2020/21 simba walichukua mataji yote  ya ndani ligi kuu, Azam Federation Cup, Ngao ya jamii na kufika robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa  Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here