Home SPORTS BILIONI 1.6 KUCHAGIZA TAIFA STARS KUFUZU KOMBE LA DUNIA QATAR 2022 –...

BILIONI 1.6 KUCHAGIZA TAIFA STARS KUFUZU KOMBE LA DUNIA QATAR 2022 – MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadau wa mpira wa miguu nchini kwenye ukumbi wa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadau wa mpira wa miguu nchini kwenye ukumbi wa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Novemba 4, 2021. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wilfred Kidau, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Yusuph Singo, Mkurugenzi Mkuu wa GSM, Gharib Mohamed na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM Mhandisi Hersi Said.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania pamoja na wadau wa soka nchini kuungana kwa pamoja na kuhakikisha timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa Miguu (Taifa Stars) inafanya vizuri kwenye michezo yote iliyobaki ili kufuzu kushiriki kombe la Dunia litakalofanyika nchini Qatar 2022.

Ametoa wito huo leo (Alhamis, Novemba 4, 2021) wakati akiongoza Kikao cha pamoja cha wadau wa soka Nchini katika ukumbi wa uwanja wa Taifa wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Ambapo katika kikao hicho wadau wa Taifa Star wamechangia Shilingi Bilioni 1.6 ambazo zitatumika kuihudumia timu katika maandalizi ya mechi zilizobaki za kufuzu kombe la Dunia.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Mheshimiwa Majaliwa amesema ni lengo la Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anakuza sekta ya michezo nchini na anataka kuona mafanikio katika timu za Taifa hivyo mikakati ya kuifanya timu ya Taifa ifanikiwe ni sehemu ya kutimiza malengo ya Mheshimiwa Rais.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda, Taasisi za Umma na binafsi pamoja na wadau wengine kuendelea kujitokeza kuichangia timu ya Taifa ili iweze kuweka Historia ya kushiriki kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

Wadau Walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na GSM, TAIFA GAS, AZAM, CRDB, NBC, LAKE OIL, STAR OIL, K4 SECURITY, KAMBIASO pamoja na wadau wengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here