Home SPORTS AZAM YAIZIBUA MTIBWA 1-0

AZAM YAIZIBUA MTIBWA 1-0


 
Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

Kikosi cha Azam leo wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Katika mtanange uliokuwa wa ushindani huku katika dakika za kipindi cha kwanza hakuna timu iliyoona lango la mwenzake .

Huku katika dakika za 52  mshambuliaji Idris Mbombo alifanikiwa kuipatia timu yake bao ambalo limedumu katika dakika zote 90.

Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 10 na kusogea nafasi ya sita, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake mbili baada ya timu zote kucheza mechi saba na kuendelea kushika mkia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here