Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya nzega mkoani Tabora imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela mkazi wa Kijiji cha wita kata ya ndala mkoani hapa Maganga Antoni (30) baada ya kupatikana na mkosa mawili ya unyang’anyi kutumia silaha na ulawiti.
Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa wilaya ya nzega Mhere Mwita alisema kutokana na ushahidi usioacha Shaka uliotolewa mahakamani hapo mahakama hiyo imeridhia kumuhukumu kifungo cha miaka 30 jela
Alisema ushahidi uliotolewa mahakamani hapo mahakama hiyo imeridhia adhabu hiyo ya kifungo cha miaka 30 jela na kuongeza kuwa adhabu hiyo iwe fundisho kwa watu wengine kwenye nia kama hiyo.
Kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo hakimu Mhere Mwita alielezwa na wakili wa serikali Jenipher Mandago aliambia mahakama hiyo kuwa mnamo mwezi wa sita ya Tarehe 5 mwaka huu 2021 majira ya usiku huko katika Kijiji cha Ntoba kata ya Ndala wilaya ya nzega na mkoa huu wa Tabora Maganga Antoni alivamia nyumba ya mwanamke mmoja jina limeifadhiwa mkazi wa Kijiji hicho na kuiba kiasi cha 42 ,000/ na kisha kumbaka mwanamke huyo kwa kumlawiti.
Wakili huyo wa serikali aliongeza kwa kusema kutokana na kitendo hicho cha kinyama alichokifanya aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine.
Hata hivyo hakimu wilaya ya nzega alitoa nafasi ya utetezi kwa Maganga Antoni kabla ya kutiwa hatiani aliomba kupunguziwa adhabu kutokana na kuwa na umri mdogo na familia inayomtegemea .
Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya nzega aikuridhia na utetezi huo na ikamuhukumu Maganga Antoni kutumikia kifungo hucho cha miaka 3o jela ambapo atakitumikia kifungo hicho kwa wakati mmoja.
Mwisho.